Majina 14 ya Wajumbe waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.


Mwenyekiti wa CCM Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akipigira kura kuchagua
wajumbe wa Kamati kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa katika
 ukumbi wa White House uliopo
makao makuu ya CCM mjini
Dodoma .
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake cha siku mbili Februari 10 na 11, 2013 kilichofanyika mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine kimeridhia uteuzi na kufanya uchaguzi wa Wajumbe 14 wa Kamati Kuu yake. 



Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dokta Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM. 



Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-



Wajumbe wa Kamati Kuu - Bara.


1. Ndugu Pindi Chana - Mbunge wa Viti Maalum.

2. Ndugu Adam Kimbisa - Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma.

3. Ndugu William Lukuvi - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge).

4. Dokta Emmanuel Nchimbi- Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

5. Ndugu Jerry Slaa - Meya wa Manispaa ya Ilala.

6. Profesa Anna Tibaijuka- Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

7. Ndugu Stephen Wassira - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu).


Wajumbe wa Kamati Kuu - Zanzibar.


Baadhi ya wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
 wakipiga kura zao kuwachagua
wajumbe wa Kamati kuu
mjini Dodoma katika
ukumbi wa White House
 
1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha- Waziri wa Ulinzi.

2. Ndugu Hussein Mwinyi - Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa - Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

4. Dokta Salim Ahmed Salim

5. Ndugu Maua Daftari - Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano na Uchukuzi.

6. Ndugu Samia Suluhu Hassan-

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)

7. Ndugu Hadija H. Aboud.



Wajumbe hao wapya wanaunda Kamati Kuu pamoja na wengine wanaoingia kwa nyadhifa zao.



Imetolewa na:-   
       
Nape Moses Nnauye,


KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI

12/02/2013

Post a Comment

أحدث أقدم