Wachezaji
wa timu ya taifa ya Mali wakishangilia baada ya kufanikiwa kuifunga
Afrika kusini kwa njia ya penati katika mchezo wa pili wa robo fainali
ya michuano ya mataifa ya Afrika.
Mlinda mlango
wa Mali Soumaila Diakite aliibuka shujaa usiku wa jana baada ya kufanikiwa
kudaka penati mbili ambazo zilipelekea matokeo ya ushindi wa penati 3-1 dhidi
ya waandaji wa fainali za mataifa ya Afrika Afrika kusini na kuivusha Mali
mpaka katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Kabla ya
penati hizo kupigwa, mchezo huo uliingia katika dakika 30 za nyongeza matokeo
yakiwa ni 1-1 na baadaye dakika 120 kumalizika bila kupatikana mbabe.
Tokelo
Rantie aliwapa uongozi Afrika kusini kwa bao la dakika ya 31 ya mchezo ambao
umepigwa katika dimba la Mabhida kabla ya nahodha Seydou Keita wa Mali
kusawazisha dakika ya 12 ya kipindi cha pili.
Siphiwe
Tshabalala alianza kuandika bao kwa penati yake nzuri ya kwanza kabla ya Cheick
Diabate kufunga penati ya kwanza kwa Mali. Furman na penati zao zilidakwa na
mlinda mlango wa Mali Diakite ilihali penati za Adama Tamboura na Mahamane
Traore wakifanikiwa kufunga penati zao kabla ya Majoro wa Afrika kusini kupiga
pembeni penati yake na kufanya matokeo ya penati kuwa 3-1 hivyo Mali kufanikia
kufuzu.
GHANA 2 CAPE VERDE 0 |
إرسال تعليق