Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimshika kwa
furaha mtoto aliyezaliwa tarehe 5.7.2013 katika hospitali ya Mkoa wa
Lindi, Sokoine huku mama wa mtoto huyo Muksim Issa ,19, anayetoka katika
kijiji cha Mumbu kilichoko katika wilaya ya Lindi vijijini aliyelala
kitandani akitabasamu. Mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 3.9
Mama Salma alitembelea hospitalini hapo kukabidhi vifaa vya hospitali
tarehe 6.2.2013. Aliyesimama kulia kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa
wa Lindi Dr. Nasoro Hamid.
Kikundi cha utamaduni
kikiwatumbuiza waalikwa kwa ngoma ya Tambiko inayochezwa na watu wa
kabila la Wamakonde wakati wa sherehe ya kukabidhi vifaa vya tiba kwenye
hospitali kuu ya mkoa wa Lindi, Sokoine, tarehe 6.2.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwahutubia viongozi na wafanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Lindi,
Sokoine,na wananchi waliohudhuria sherehe ya kukabidhi rasmi vifaa vya
tiba kwenye hospitali hiyo tarehe 6.2.2013 huko Lindi Mjini. Waliokaa
kushoto kwa Mama Salma ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali Dr.
Nicolaus Munni, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ambaye pia ni Meya wa
Lindi Mjini Ndugu Frank Magali na wa mwisho ni Mwakilishi wa Project
C.U.R.E. nchin Tanzania Bwana Makembe Kimario.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi kwa vifaa vya hospitali ya mkoa
wa Lindi,Sokoine, vilivyotolewa na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na
Shirika la Project C.U.R.E. la nchini Marekani. Vifaa hivyo vina thamani
ya zaidi ya shilingi milioni mia saba. Kulia kwa Mama Salma ni Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Dr. Nasoro
Hamidi akifuatiwa na Katibu wa CCM WA Mkoa huo Ndugu Adelina Gefi na
kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali Dr. Nicolaus Munni.
Sherehe hiyo ilifanyika tarehe 6.2.2013.
Post a Comment