>>NAPOLI YANYUKWA KWAO 3-0, BENFICA, UGENINI, YAIWASHA LEVERKUSEN!
KATIKA
Mechi za kwanza za EUROPA LIGI za Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Chelsea,
ambao walishindwa kutetea Taji lao la Ubingwa wa Ulaya na kubwagwa
EUROPA LIGI, leo wameanza vyema Michuano ya EUROPA LIGI ugenini kwa
kuifunga Sparta Prague Bao 1-0 lakini wenzao Liverpool, wakicheza huko
Urusi, walipigwa Bao 2-0 na Zenit St Petersburg.
Huku kukiwa bado kuna Mechi nyingine
zinazochezwa leo, katika Mechi zilizoanza mapema Napoli walinyukwa Bao
3-0 wakiwa kwao na Viktoria Plzen na Benfica, wakicheza ugenini,
kuifunga Bayer Leverkusen Bao 1-0.
SPARTA PRAGUE 0 CHELSEA 1
Oscar, alietokea Benchi, ndani ya
Sekunde 45, alifunga Bao 1 na la ushindi na kuisaidia Chelsea kushinda
ugenini Bao 1-0 walipocheza na Sparta Prague.
Oscar alipata Bao hilo kufuatia ushirikiano na ujanja wa Edin Hazard aliempa pande kwa kisigino.
Licha ya kutocheza vizuri na kutengeneza
nafasi chache, Chelsea sasa wapo katika nafasi nzuri kwa Mechi ya
Marudiano kwao Stamford Bridge hapo Februari 21.
VIKOSI:
Sparta Prague: Vaclik, Zapotocny, Svejdik, Holek, Hybs, Husbauer, Vacha, Matejovsky, Kadlec, Lafata, Krejci
Akiba: Cech, Pamic, Kweuke, Vidlicka, Polom, Bednar, Janos.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Bertrand, Lampard, Ramires, Marin, Mata, Hazard, Torres
Akiba: Turnbull, Cole, Oscar, Ferreira, Terry, Benayoun, Ake.
Refa: Daniele Orsato (Italy)
ZENIT ST PETERSBURG 2 LIVERPOOL 0
Liverpool walikosa nafasi za wazi na
kujikuta wakiadhibiwa kwa Bao za ndani ya Dakika 3 za Mbrazil Hulk na
Sergei Semak zilizowapa Zenit St Petersburg ushindi wa Bao 2-0
walipocheza Nyumbani Uwanja wa Stadion Petrovski, St Petersburg, Urusi.
++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Zenit St Petersburg 2
-Hulk Dakika ya 70
-Semak 72
Liverpool 0
++++++++++++++++++++++
Luis Suarez alikosa nafasi kadhaa za wazi na hilo liliwafanya Liverpool wakose ushindi.
VIKOSI:
Zenit St Petersburg: Malafeev, Aniukov, Luis Neto, Lombaerts, Hubocan, Shirokov, Denisov, Witsel, Hulk, Kerzhakov, Danny
Akiba: Zhevnov, Faitzulin, Rodic, Lukovic, Semak, Djordjevic, Evseev.
Liverpool: Reina, Johnson, Skrtel, Carragher, Jose Enrique, Gerrard, Allen, Henderson, Downing, Suarez, Sterling
Akiba: Jones, Coates, Lucas, Borini, Fernandez Saez, Shelvey, Wisdom.
Refa: Carlos Velasco Carballo (Spain)
RATIBA/MATOKEO:
RAUNDI ya MTOANO TIMU 32:
Alhamisi Februari 14
Zenit St Petersburg 2 Liverpool 0
Anzhi Makhachkala 3 Hannover 1
BATE Borisov 0 Fenerbache 0
Levante 3 Olympiakos 0
Dynamo Kiev 1 Bordeaux 1
Bayer Leverkusen 0 Benfica 1
Ajax 2 Steaua Bucharest 0
Sparta Prague 0 Chelsea 1
Napoli 0 Viktoria Plzen 3
[Saa 5 Dak 5 Usiku]
Atletico Madrid v Rubin Kazan
Borussia Monchengladbach v Lazio
Tottenham v Lyon
Basel v Dnipro
Inter Milan v Cluj
Newcastle v Metalist Kharkiv
Stuttgart v Genk
RATIBA ya MECHI:
Mechi ya 1=14 Februari 2013
Mechi ya 1=21 Februari 2013
RAUNDI ya MTOANO TIMU 16:
**Mechi kuchezwa Machi 7 na Marudiano Machi 14
Napoli or Viktoria Plzen v BATE Borisov or Fenerbache
Leverkusen or Benfica v Dynamo Kiev or Bordeaux
Anzhi Makhachkala or Hannover v Newcastle or Metalist
Stuttgart or Genk v Monchengladbach or Lazio
Tottenham or Lyon v Inter Milan or Cluj
Levante or Olympiakos v Atletico Madrid or Rubin Kazan
Basel or Dnipro v Zenit St Petersburg or Liverpool
Ajax or Steaua Bucharest v Sparta Prague or Chelsea
RATIBA ya MECHI:
Mechi ya 1=7 Machi 2013
Mechi ya 2=14 Machi 2013
+++++++++++++++++++
RATIBA HATUA YA MTOANO
RAUNDI YA TIMU 32:
Mechi ya 1=14 Februari 2013
Mechi ya 1=21 Februari 2013
RAUNDI YA TIMU 16:
Mechi ya 1=7 Machi 2013
Mechi ya 2=14 Machi 2013
ROBO FAINALI:
Mechi ya 1=4 Aprili 2013
Mechi ya 2=11 Aprili 2013
NUSU FAINALI
Mechi ya 1=25 Aprili 2013
Mechi ya 2=2 Mei 2013
FAINALI
15 Mei 2013
UWANJA wa AMSTERDAM ARENA

إرسال تعليق