Mizozo ya kisiasa chanzo cha kuzorota kwa Haki za binadamu duniani.

Wawakilishi  wa kundi la kutetea haki za binadamu- Human Rights Watch, wanasema  katika ripoti yao ya kila mwaka kwamba wana wasiwasi juu hali nchini Syria, Mali na nchi nyingine za kiarabu. Kundi hilo lenye makao yake New York lilitoa ripoti hiyo Alhamis  katika miji ya London na Johannesburg.
 Human Rights Watch linasema maandamano ya umma yaliyotokea katika nchi za kiarabu miaka miwili iliyopita hayakuimarisha  haki  kwa raia. Katika ripoti yake ya kurasa  665 iliyotolewa Alhamis kundi hilo linaelezea hali ya haki za binadamu katika nchi 80 ikiwemo Marekani, huku mzozo wa Syria ukiangazwa zaidi kwenye ripoti hiyo ambapo zaidi ya watu elfu 60 wamepoteza maisha yao.
Tiseke Kasambala mkurugenzi  wa kundi hilo tawi la Afrika anasema hali barani humo nayo inazidi kuleta wasiwasi.  “Mwaka wa 2012 ulishuhudia kuporomoka kwa maendeleo ya kidemokrasia  na haki za binadamu  pamoja na tishio la ugaidi katika nchi za Nigeria,  Somalia na Kenya.”
  Kasambala anasema mzozo unaoendelea Mali, Sudan na Sudan Kusini na vita katika  Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo pamoja na Ethiopia na Eritrea, unahujumu maendeleo yaliyopatikana.

Post a Comment

Previous Post Next Post