MSANII WA KUNDI LA WANAUME HALISI AFARIKI DUNIA(BK)

Msanii na mmoja wa waasisi  wa kundi la Wanaume Halisi Baraka Masale au "BK"  Pichani amefariki Dunia leo katika hospitali ya Muhimbili. BK alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo kwa muda mrefu. Mungu ailaze mahala pema peponi Roho ya Marehemu.
Leo alfajiri game ya muziki wa kizazi kipya imempoteza nyota wake ambaye alikua member wa kundi la TMK Wanaume halisi.The late Baraka Sekela, kwa jina la stage ni BK, ambaye yeye ni moja kati ya waasisi wa kundi la TMK Family, hata makao makuu ya kundi hilo yalikua nyumbani kwa wazazi wake karibu na uwanja wa taifa wilaya ya Temeke, jijini dar es salaam.Marehemu bk alikua anaumwa, hadi mauti yanamkuta alikua amelazwa hospitali ya rufaa ya muhimbili.
"Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu sana Hassan Omandi, marehem alikua anaumwa tumbo kwa takribani siku tisa na kuambiwa ana taifod katika hospitali aliyoenda kufanya vipimi, lakini baada ya kuanza dozi akazidiwa kabisa, ikabidi twende hospitali ya Temeke, kule wakaona ni tatizo kubwa na kumpeleka Muhimbili, ndio huko akaambiwa ini lake linamatatizo ya kuvimba."amesema rafiki yake wa karibu anaeitwa Hassan Omande 
 

 Juma nature ni moja kati ya wasanii waliowahi kufanya kazi kwa karibu na BK wakati wa uhai wake,nae amezungumza


Sauti ya bk iliwashi kuskika kwenye sitaki dem rmx ya juma nature. SIKILIZA HAPA CHINI 

Juma nature pia alizungumza kuhusu swala zima la mazishi

Post a Comment

أحدث أقدم