Menejawa
Ubunifu wa ofa za Tigo David Sekwao (katikati) akizungumza na mshindi
wa droo ya promosheni ya Tigo Smart Card kupitia simu ya kiganjani
jijini Dar leo. Anayeshuhudia tukio hilo Kulia ni Ofisa Mkaguzi kutoka
Bodi ya Taifa ya kusimamia michezo ya kubahatisha.
Tigo
Tanzania leo imetangaza mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya
smartcard kuwa ni Bwana Julius Raphael Kanza ambaye ni mkazi wa jiji la
Dar es Salaam.
Bwana
Kanza ameshinda zawadi kuu ambayo ni tiketi ya bure ya kwenda na kurudi
Madrid Uhispania pamoja na kulipiwa gharama zote za safari kwenda
kutizama mechi ya soka kati ya Real Madrid na FC Barcelona.
Alivyojulishwa
kuhusu ushindi wake Bwana Kanza alifurahishwa sana na kusema
“sikutegemea kabisa kuwa mshindi wa droo hii, nimefurahi sana na
ninajiona wa muhimu sana. Napenda kuwashukuru Tigo kwa zawadi hii na
nina hamu sana siku ziwadie niende kushuhudia mechi hii kubwa kati ya
Real Madrid na FC Barcelona”.
“Droo
hii ni mwendelezo wa droo za promosheni ya smartcard ambazo zinaendelea
kufanyika kila mwezi, robo mwaka, na kila mwaka. Promosheni ya
smartcard ilizinduliwa Septemba 2012 hususan kwa ajili ya wateja wa Tigo
ambao wanatumia smartphones kama Blackberry, Android na iphone.”
Alisema Bwana David Sekwao meneja wa ubunifu wa ofa za Tigo.
Bwana
Sekwao aliendelea kwa kusema kuwa “Mbali na zawadi kuu ya droo hii,
washindi 42 watabahatika kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo tiketi
12 za sinema, tiketi 12 za klabu, tiketi 12 za kuangalia mechi za mpira
kwenye klabu ya hapa nchini, vocha 3 za kununua bidhaa mbalimbali na
vocha 3 za chakula cha jioni.” Aliongeza kuwa “mshindi wa leo bwana
Kanza atapatiwa tiketi ya bure ya kwenda na kurudi Madrid Uhispania na
kulipiwa gharama zote za safari kwenda kuangalia mechi ya soka kati ya
Real Madrid na FC Barcelona ambazo ndio timu kuu za ligi ya Hispania La
Liga”
Kushiriki
katika shindano hili, mteja alitakiwa awe amejiunga na kifurushi cha
Smartcard chenye thamani ya Tshs 30,000 kwa mwezi na awe ametumia huduma
hii kwa miezi mitatu mfululizo na vilevile awe amejiunga na jamii ya
smartcard kupitia www.tigo.co.tz/smartcardcommunity
Zawadi
nyingine kuu za mwaka za droo hii ni pamoja na tiketi ya ndege ya
kwenda na kurudi Dubai, malazi ya siku 5 pamoja na hela ya matumizi
kiasi cha shilingi laki moja na nusu kwa siku na vilevile tiketi na
gharama za kwenda na kurudi Uingereza kuangalia mechi kati ya Arsenal na
man United mwezi Aprili mwaka 2013.
Post a Comment