EXCLUSIVE INTERVIEW NA KALA JEREMIAH KUHUSU MUZIKI NA MAISHA.


HZB: Majina yako kamili unaitwa nani?
 KALA: Kala Jeremiah Masanja.

HZB: Kwa nini umeamua kutumia jina lako kamili na siyo nick name?
KALA: Ujue me nimetokea bongo star seach na kule ulikua unaandikisha majina yote kamili sasa watu kuwabadilishia jina tena naona kama na wachanganya.

HZB: Nini maana ya 044
KALA: Ni saa kumi na dakika arobaini na nne (04:44).

HZB:Ilitokea nini 04:44?
KALA: Hahaha ilitokea nini? watu wakitaka kujua hii 04:44 wanunue album yangu nimeelezea .


HZB: Ni shule gani ambazo umepita?
KALA: shule ya msingi nimesoma shule kama mbili hivi tofauti, Kinango pamoja na Mendo, secondary nimesoma Donbosco,.baada ya hapo nikaingia kwenye  game ya music.

HZB: Umeanza game rasm lini? Na ngoma ipi?
KALA: Nilianza tangu mwaka 2004, nikatoa ngoma moja inaitwa Dunia ya matangazo nilifanyia studo za Mwanza. Kasha 2006 nikaingia bongo star seach.

HZB: Kipindi unakua ulijua kama utafanya music?
KALA:Hapana sikujua kabisa kama ntafanya music yaani sikujua kabisa kama ntakuwa mwana mziki mi nimeanza tu kujisitukia mwenyewe mwaka 2004 nimeanza kupenda muziki ndo nikaandika vesi langu sasa.

HZB: Nani ambaye alikushawishi kufanya muziki kwa kipindi hicho?
KALA:Wako wengi tu sana  wan je wa bongo, ila wa bongo nilikua na  album nyingi tu kama nne nilikua na album ya Jay moo ya kwanza, nilikua na album ya Prof jay ya kwanza nilikua na album ya Waswahili ya kwanza, na nilikua na album ya mwana FA. Lakini album ya waswahili nilikua nasikiliza sana hata ngoma zangu za mwanzo nimefanya kama wale jamaa,waliimbaga pengo yupi bora kati ya rafiki, yani vile walivyokuwa wanasimamia mada wanaichambua mada nilikua napenda sana.

HZB: Ni mafanikio gani umeyapata tangu uanze game hii ya muziki?
KALA:aaaah mafanikio kwenye muziki yapo mengi ingawa mengine siyo ya moja kwa moja, unajua kupitia muziki nimejulikana na kujulikana kumenisaidia meni nimepata vitu vingi sana tofauti na muziki,naheshimiwa na watu mbalimbali kama wazee, watoto, vijana.na wakati mwingine mzee akikuona ankuita anakua anakuelezea matatizo yake ili niyafikishe kwa jamii, soo nafarijika sana.

HZB:Ulisha wahi kukutana na mzee alfu akaimba hata mistari miwili katika moja ya ngoma zako?
KALA: Yaaaa wapo wengi tu sana ujue me muziki ninao fanya unakubalika na watu wengi,na hata ushari mwingi nachukua kwa wazee coz wao wanajua vitu vingii sana kwa hii nchi.

HZB:Mashabiki wako unawahaidi nini kwa mwaka huu wa 2013?
KALA: Watarajie vitu vingi tu sana kama wanavyojua Kala ni mtu wa jamii so navitu vingi sana kwa ajili yao, ninaproject za kijamii nataka kuzifanya mwaka huu,nitafanya mengi sana ya kijamii kwa ajili ya maendeleo ya kitaifa na familia.

Wa mwisho kushoto ni Mama ake mkubwa, anaefuata Mama mzazi na Bibi


HZB: Wasanii wengi kwa sasa wamekuwa wakitoa single tu na siyo album, je unahisi album hazilipi?
KALA:aaa muziki sasa hivi umeamia kwenye show, ujue digitali kama digitali yaani teknolojia imeleta hasara nyingi lakini pia imeleta faida nyingi, ujue sasahivi flash nyingi, memory card nyingi, sasa mtu anawekewa tu nyimbo hata yale mauzo ya album inakua siyo sana kama zamani, unajua sisi zamani kama nilivyokuambia nilikua na album nne kwahiyo ulikua kupata album kama ya Prof jay lazima unanunua tape zile bamboo ya kuban haya kuwepo.

HZB: Kama album hailipi mbona wewe tayari umeachia album.
KALA:Hizo ni ndoto zangu kama msanii nilikua nazo toka zamani nije kufanya album ili mashabiki wangu ambao wanapenda kupata nyimbo zangu zote wasipate tabu.wakati nilikua natengeneza album sikufikiria sana pesa nilifikiria mashabiki wangu coz wengine walikua wananisikiliza kwenye radio tu hwanielewi, soo kupitia hii album nahisi nitaongeza mashabiki.
album ya Kala


HZB: East Africa ni msanii gani unatamani kufanyanae kazi?
KALA: Aaah wengi sana bro nikiwataja tutajaza ukurasa acha niseme wengi tu, wote wanaofanya vizuri.

HZB: Ni producer gani unamkubali hapa bongo?
KALA: Mimi sina producer ambaye nimemkalili producer yeyote tu nafanyanae kazi, hata album yangu ukiangalia kila wimbo unaproducer wake,unaona kama dia God nimefanya na producer D classic ambaye alikua bado hajajulikana lakini goma ndo kama hilo unalisikia.
D Classic


HZB:Tukirudi nyuma kidogo ni haso gani umepitia kufanya ngoma yako ya kwanza?
KALA:Wimbo wangu wa kwanza haukunipa tabu sana kurecord coz nilitumia bit ya mtu niliipenda nikamwambia naomba nitumia bit yako, nikaenda studio nilikua nimefanya mazoez na nilikua najua hakunaga kukosea, ukikosea umeharibu wimbo mzima, soo nikafanya mazoez ya kutosha na siku naingiza mpaka Yule producer akashangaa na likua narecord kwa lengo la kusikiliza mimi wala sikua nafikiria kufanya muziki lakini watu walivyokua wanasikiliza wakawa wananishawishi.


HZB: Ni ngoma gani katika ngoma zako unaikubali?
KALA: aah ninazo nyingi sana za Kala jeremiah?.. nina red  to die, ningekuwa rais, wizi mtupu yaani magoma hayo nikiyasikia nawehuka kabisaa.

HZB: Ushauri wako kwa wasanii wanao anza muziki?
KALA: Ushauri wangu kwanza wajiamini, pia waangalie kitu ambacho wanaiba yaani maada inabidi watufute mada nzuri ndo itakayo wafikisha mbali, kama kuchana kuna watu wanachana ile mbayaa.

HZB: Neno la mwisho kwa mashabiki wako?
KALA:Mashabiki wangu nawapenda sana coz bila wao mimi nisinge kuwa Kala Jeremiah unaemfahamu wewe,

UNAWEZA KUSIKILIZA MAZUNGUMZO HAPO CHINI.
 

Post a Comment

Previous Post Next Post