MTIBWA NA YANGA KATIKA PICHA LEO WALIVYOTOANA JASHO YA 1 - 1 TAIFA,

Mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Kiiza akifumua shuti mbele ya beki wa Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka 1-1.


Kiiza akijiandaa kupiga shuti

Kipa Hussein Sharrid 'Casillas' wa Mtibwa Sugar akizuia mchomo wa mshambuliaji wa Yanga SC, Jerry Tegete

Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya akimtibu kiungo wa Yanga, Simon Msuva baada ya kuumia katika moja ya pilika za mchezo huo

Kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kisiga 'Malone' akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Yanga, Athumani Iddi 'Chuji' na Mbuyu Twite kulia

Wachezaji wa Mtibwa wakimpongea Kisiga baada ya kuifungia timu yao bao la kuongoza leo

Kikosi cha Mtibwa leo

Kikosi cha Yanga leo

Hamisi Kiiza wa pili kutoka kushoto na Said Bahanuzi kabla ya kuingia kuinusuru Yanga leo
  
Kipa Hussein Sharrif 'Casillas' akiwa ameruka juu kuokoa moja ya hatari langoni mwake

Casillas anampokonya mpira miguuni Tegete akienda kufunga

Simon Msuva wa Yanga kushoto akimtoka beki wa Mtivwa

Didier Kavumbangu alifanikiwa kumlamva chenga Casillas, lakini akapiga nje

Kavumbangu anamlamba chenga Casillas

Tegete chini ya ulinzi mkali wa mabeki wa Mtibwa

Tegete ameacha mpira, baada ya Casillas kuuzuia

Beki wa Mtibwa, Salum Swedi akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbangu 

Beki wa Mtibwa, Said Mkopi akiondosha mpira kwenye hatari mbele ya mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Kiiza

Kiungo wa Yanga, Frank Domayo akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Mtibwa, Rashid Gumbo

Haruna Niyonzima akiondoka na mpira mbele ya mchezaji wa Mtibwa

Casillas hapa anazuia mchomo wa Msuva

Shaaban Nditi akitafuta mbinu za kumpokonya mpira, Haruna Niyonzima mbele

Msuva akimtoka Issa Rashid 'Baba Ubaya'

Mpira umetulia nyavuni, bao la Mtibwa huku wachezaji wa Yanga wakilaumiana na kipa wao
Picha na Bin Zubeiry blog
Casillqas akiwalalamikia mabeki wake, mpira uko nyavuni mfungaji Kiiza anaanza kushangilia akisindikizwa na Tegete

Post a Comment

أحدث أقدم