NAKANUSHA HABARI ZA UONGO

Msanii Linah Sanga siku alipokua Boston, Massachusetts nchini Marekani

Msanii wa kizazi kipya Linah Sanga amekanusha habari zilizotoka kwenye mitandao ya kijamii kwamba  anatoka kimapenzi na KIJANA aliyejipatia umaarufu kwa 'kumvamia' msukuma kabumbu wa Real Madrid, ‘Kaka’ Nagari Kombo. 

Linah amekanusha vikali kuhusu habari hiyo na kukemea mitandao inayoandika habari za mtu bila ya kuhakikisha kwanza, aliendelea kwa kusema maisha ya mahusiano ni 'Private Life' ya msanii, na kama kuna ulazima wa kuwekwa hadharani basi msubiri msanii mwenyewe aongee, hata kama umesikia kitu na huna uhakika nacho, kwanini usimuulize muhusika kusudi upate kusikia upande wa pili wa stori unasemaje.

Msanii huyo wa kizazi kipya amelaani vikali habari hiyo na kuongezea Nagari Kombo ni rafiki yake na sio kwamba ndiye anayemmiliki kimapenzi, mimi ni SINGLE naomba muelewe hivyo na kama kuna lolote si msubiri muambiwe jamani?

Post a Comment

Previous Post Next Post