![]() |
DAR ES SALAAM,
Chama
Cha Mapinduzi-CCM-kimesema kina uhakika wa kushinda katika Uchaguzi
Mkuu ujayo wa mwaka 2015 kutokana na kwamba bado kipo imara na
kinakubalika na Watanzania wengi.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi Ndugu NAPE NNAUYE wakati akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri
Kuu ya Tawi la Ofisi Ndogo Makao Makuu na baadhi ya wanachama wa Tawi
hilo mara baada ya kufungua Ofisi Mpya ya Tawi la Ofisi Ndogo.
Kwa
imani hiyo amesema hakuna sababu ya Wana-CCM kukata tamaa kwani
wamezunguka Mikoani na kujionea hali halisi ya jinsi wananchi
wanavyoendelea kukiamini Chama tawala ambacho ni Chama cha Wakulima na
Wanyonge.
Kuhusu
migongano ya Dini Katibu huyo wa NEC, Itikadi na Uenezi amesisitiza
kuwa migongano hiyo itamalizwa na Chama kwa kushirikiana na viongozi na
wananchi kwani CCM ndicho Chama pekee chenye kudumisha amani na
mshikamano miongoni mwa Watanzania.
Mapema
akisoma risala ya wanachama wa Tawi la CCM la Ofisi Ndogo ya Makao
Makuu lililopo katika Kata ya Jangwani, Katibu wa Tawi Ndugu ROSE THOMAS
amesifu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na chama katika kurejesha
imani ya CCM kwa wananchi.
Tawi hilo la Ofisi Ndogo lina Mashina Sita na lina wanachama 308.

إرسال تعليق