Nchi 11 za Afrika zakubali mkataba wa Umoja wa Mataifa

Wapiganaji waasi wa M23 ambao wamekuwa wakitekeleza mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali ya DR Congo

Na Martha Saranga Amini

Nchi kumi na moja za Afrika zimealikwa kusaini mkataba na Umoja wa Mataifa wa mwishoni mwa juma hili kwa lengo la kukomesha vita vilivyodumu kwa zaidi ya miongo miwili huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky alisema ijumaa kuwa kiongozi wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon atafanya jitihada kupata mkataba uliosainiwa Addis Ababa jumapili.

Nesirky ameongeza kuwa kama mpango utafanikiwa utawezesha uvamizi maalum wa jeshi la umoja wa mataifa UN huko mashariki mwa Congo ili kupambana na makundi ya waasi na kusaidia utatuzi wa masuala ya kisiasa.

Msema wa umoja wa mataifa ameongeza kuwa viongozi wa DR Congo, Angola, Burundi, afrika ya kati, jamuhuri ya Congo, Rwanda, afrika kusini,Sudan kusini,Tanzania, Uganda na Zambia ni miongoni mwa mataifa yaliyoalikwa.

Maraisi kadhaa wanatarajiwa kuhudhuria.

Post a Comment

Previous Post Next Post