TAARIFA YA UHAKIKA
KABISA ILIYOIFIKIA MUDA HUU INAELEZA KUWA MAHAKAMA KUU KANDA
YA MWANZA IMEUSIMAMISHA UCHAGUZI MKUU WA TFF,BAADA YA ALIEKUWA MGOMBEA WA
NAFASI YA URAIS KWENYE KINYANG'ANYIRO HICHO,BW. RICHARD RUKAMBURA KUFUNGUA
MASHTAKA KWENYE KESI NAMBA MOJA YA MWAKA 2013,KUPINGA KUENGULIWA KWAKE KWENYE
KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI ULIOPANGWA KUFANYIKA FEBRUARI 24,MWAKA HUU.
KESI HIYO ITAANZA
KUSOMWA KWA MARA YA KWANZA FEBRUARI 19.
RUKAMBURA AMBAYE
ALIENGULIWA KWENYE HATUA ZA AWALI KABISA ZA MCHAKATO WA UCHAGUZI NA KAMATI YA
UCHAGUZI ILIYOKUWA CHINI YA NDUGU LYATO BAADA YA KUBAINIKA KUWA AMEJAZA FOMU
MBILI ZA KUWANIA UONGOZI HUKU MOJA IKIWA NI YA KUWANIA URAIS NA NYINGINE UJUMBE
WA KAMATI YA UTENDAJI.
LAKINI JANA RUKAMBURA
ALIFUNGUA KESI TATU DHIDI YA TFF,MOJA IKIWA NI KUTAKA MAHAKAMA IZUIE UCHAGUZI
NA KUPINGA KUENGULIWA KWAKE NA KUTAKA AREJESHWE KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI
HUO.
KESI YA PILI AMBAYO BADO
HAIJAPANGIWA TAREHE,ANATAKA MAHAKAMA IIZUIE TFF KUTUMIA KIGEZO CHA FIFA CHA
KUWANYIMA HAKI WATU WENGINE.NA KESI YA TATU ANATAKA TFF IMLIPE FIDIA KWA SABABU
IMEMDHALILISHA KWA KUMUENGUA KWA KIGEZO CHA KUJAZA FOMU MBILI WAKATI ANAEGOMBEA
SHARTI AGOMBEE NAFASI MOJA.
''LAKI SABA YANGU
WAMECHUKUA NA RISITI NINAZO,LAKI MBILI NILILIPA YA UJUMBE NA LAKI TANO YA
URAIS,SASA KAMA SHARTI LAO NI KUGOMBEA NAFASI MOJA KWANINI WASISEME?"
ALISEMA RUKAMBURA.
ALIENDELEA KUSEMA
''WAMENIDHALILISHA,MIMI NI MTU MZIMA NA NINA FAMILIA YANGU,NINA DIGRII TOKA
MWAKA 2004 NA NILIGOMBEA NA TENGA MWAKA 2008 WAKANIENGUA,LAKINI SAFARI HII
SIKUBALI.ALIMALIZA KUSEMA RUKAMBURA.
إرسال تعليق