
Admir Suljic, mtuhumiwa wa upangaji wa matokeo ya soka duninani, ametiwa nguvuni na Polisi ya Italia.
Mtuhumiwa huyo, raia wa Slovenia alitiwa nguvuni na mamlaka za Italia
baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Malpensa mjini Milan akitokea
Singapore.
Suljic anatakiwa na mamlaka za kisheria za mji wa Cremona nchini Italia ambao wanafanya uchunguzi wa kesi kubwa ya upangaji wa matokeo ambayo imeshapelekea kukamatwa kwa watu zaidi ya 50, huku wengine zaidi ya150 wakichunguzwa.
Suljic anatakiwa na mamlaka za kisheria za mji wa Cremona nchini Italia ambao wanafanya uchunguzi wa kesi kubwa ya upangaji wa matokeo ambayo imeshapelekea kukamatwa kwa watu zaidi ya 50, huku wengine zaidi ya150 wakichunguzwa.
Polisi ya Italia inasema kuwa Suljic amekuwa akitafutwa tangu Desembea 2011 na alikuwa "kiungo muhimu" katika Upangaji Mkubwa wa Matokeo uliopita.
Polisi inasema alitumia muda mwingi nchini Singapore akifanya mawasiliano ya karibu na vigogo wa genge maarufu la upangaji matokeo.
Mapema Alhamisi, akizungumza kwenye kongamano maalaumu nchini Malaysia
kuhusu upangaji matokeo, katibu mkuu wa polisi ya Kimataifa (Interpol),
Ronald Noble, alibainisha kuwa polisi ya Singapore ilizitonya mamlaka za
Italia kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akisafiri kwenda mjini Milan.
Singapore imekuwa chini ya shinikizo kubwa linaloitaka ichukue hatua
baada ya Polisi ya Ulaya (Europol) kuwahusisha mamia ya watuhumiwa wa
uhalifu huo duniani na mtandao uliopo nchini humo.
MTANDAO WAUHALIFU
Noble alisema kuwa mtu huyo alikuwa akitakiwa nchini Italia kwa sababu
anatuhumiwa kufanya kazi na Tan Seet Eng, mfanyabishara raia wa
Singapore, ajulikanaye kama Dan Tan, ambaye mamlaka za Italia zimetoa
kibali cha kukamatwa.
Polisi ya Italia inasema kuwa Suljic alitaka kuzikimbia mamlaka za Italia na kwamba anakabiliwa na tuhuma za magenge na mitandao ya uhalifu wa michezo.
Polisi ya Italia inasema kuwa Suljic alitaka kuzikimbia mamlaka za Italia na kwamba anakabiliwa na tuhuma za magenge na mitandao ya uhalifu wa michezo.
Mwezi Novemba, mwanasoka kutoka Serbia, Almir Gegic, ambaye alikuwa akitakiwa na mamlaka za Italia alikamatwa Malpensa.
Tan anatuhumiwa kuongoza genge la uhalifu linaloingiza mamilioni ya dola kwa kufanya kamari wakati wa mechi za mpira wa miguu nchini Italia.
Maafisa wa Italia wameshindwa kumkamata Tan kwa sababu kibali cha kumkamata hakiwezi kutumika wakati yuko Asia.
Kwa kujua kuwa Singapore imekuwa ikikosolewa sana kwa kutomkamata Tan,
Noble anasema kuwa mamlaka zilishindwa kwa sababu zililazimika kufuata
sheria zao na wangechukua hatua kama wangekuwa na ushahidi wa kutosha.
Hata hivyo, Noble aliongeza kusema kuwa wapelelezi duniani kote wamekuwa wazito kuwakamata wapangaji wa matokeo ya mechi kwa sababu mpaka sasa "hawajawa na maandalizi ya kutosha kufanya kazi kwa pamoja" na kubadilishana taarifa na wenzao wa kimataifa.
Ralf Mutschke, mkuu wa usalama wa FIFA, akizungumza katika kongamano
hilo la Malaysia, alisema kuwa ana matumaini kuwa bwana Tan atakamatwa
na kupelekwa mbele ya mahakama kwa msaada wa mamlaka za Singapore.
NAFASI YA SINGAPORE
Kwa upande wao, Polisi ya Singapore inasema kuwa bwana Tan "anaisaidia" Polisi katika uchunguzi.
Tan, ambaye amekuwa aktajwa katika uchunguzi mbalimbali na kutakiwa
nchini Italia licha ya kukanusha tuhuma dhidi yake, "kwa sasa
anazisaidia mamlaka za Singapore katika upelelezi wao", ilisema taarifa
ya polisi.
Ni mara ya kwanza polisi kusema kuwa Tan anaendelea kuhojiwa. Vilevile
polisi wamethibitisha kuwa wao ndio waliotoa taarifa zilizopelekea
kukamatwa kwa Sulic.
"Mamlaka za Singapore zimekuwa zikitoa msaada na ushirikiano na nchi
zilizoathirika na itaendelea kufanya hivyo," ilisema taarifa hiyo.
Jeshi la Polisi la Singapore limetangaza kuwa maafisa wanne waandamizi
wa jeshi hilo na Taasisi ya Kupambana na Rushwa (CPIB) wataelekea makao
makuu ya Interpol mjini Lyon, Ufaransa, kuungana na kikosi kazi cha
kupambana na Upangaji Matokeo duniani.
Mshirika wa zamani wa Tan, Wilson Raj Perumal, amewaambia wapelelezi wa Italia kuwa Tan has alleged to Italian investigators that Tan aliweka shuruti za malipo kwenye mechi husika kwa kutumia mitandao yenye makao inayosimamiwa nchini China.
Ripoti iliyotolewa na polisi ya Umoja wa Ulaya mapema mwezi huu ilisema kuwa magenge ya uhalifu, yakiwemo kutoka Asia, yalipanga au kujaribu kupanga matokeo ya mamia ya mecho za mchezo wa soka duniani kote.
Europol ilisema kuwa uchunguzi wake wa miezi 18 ulibaini kuwepo kwa mechi 380 zinazotuhumiwa kupanga matokeo barani Ulaya na michezo mingine 300 yenye kutia shaka nje ya bara la Ulaya, hususan Afrika, Asia, Kusini na Katikati mwa Amerika.
Post a Comment