
Omotola na mume wake watatu kutoka kushoto wakiwa na familia yao mwaka 2012.
Baada ya kuingia kwenye headlines na kukanusha kwamba hajafanyiwa
opareshen ya kuondoa nyama zilizozidi tumboni kwake, mwigizaji Mnigeria
Omotola Jalade ambae amewahi kuja bongo kuzindua movie mpya ya Wema
Sepetu, ameingia tena kwenye headlines.
Sasa hivi amehusishwa na taarifa za kuaminika kwamba amekua akimpiga
mumewe aitwae Mathew Ekeinde, na hiyo hutokea mara kwa mara pale
wanapokosana.
Stori inaendelea kutiririsha kwamba pamoja na tabia hiyo aliyonayo
Omotola, Ekeinde amekua mvulivu na mwenye busara na amejizuia sana
manake hajawahi kumpiga hata siku moja kwa sababu anampenda sana.
Omotola kweli anahulka ya kibabe, nakumbuka wakati alipokuja bongo
nilipata nafasi ya kuingia kwenye chumba chake alichokua analala,
nilikwenda kumfanyia interview… nilishuhudia jinsi alivyokua
akimuendesha Cameraman wake kibabe, pia alimzodoa kibabe mbele ya watu
kijana mmoja ambae alimkubalia kupiga picha lakini kijana akamshika
Omotola kiunoni, ghafla mwigizaji huyo akabadilika na kumuwakia kwamba
asimfananishe na madem wa saizi yake, hatakiwi kumshika hivyo.
إرسال تعليق