
Jana kupitia mtandao wa Twitter mwanadada Lady Jaydee alisimulia
kitendo kilimchokera baada ya polisi walioitwa kwenda kumsaidia akiwa
kwenye chumba cha hoteli baada ya kuzidiwa ambao waliamua kuwapigia simu
waandishi wa habari za udaku waje wapate picha na habari.
“Police mnatumwa kuja kuni rescue mgonjwa Hotel Room, mnaita
waandishi waje kuchukua story! Hamjanitendea haki, nimesikitishwa,”
alitweet Jaydee.
“Nawaambia I can’t walk wananilazimisha shuka watu watakubeba gari tumepaki nyuma. Kumbe camera ziko chini huko zinangoja.”
Akijibu swali lililouliza kama waandishi hao walipata
walichokitaka Jaydee alijibu, “I told them walete doctor humo hotel room
kama hawawezi waondoke. Hotel staff told me nsishuke kuna camera chini.”
“Mwenyewe nashangaa hawakuwa wanajali mimi kupata nafuu bali maslahi. Hakuna utu hapo.”
Alimalizia kwa kuandika, “Hamtujali, na hamjali lolote. Kila mtu ana
shida zake ila msichukulie advantage kutunyima haki zetu za msingi.
Nimeumia sana!
Hata hivyo Jaydeea alidai kuwa kwa sasa anaendelea vizuri ingawa
hatukuweza kufahamu alikuwa hoteli gani na wapi pamoja na tatizo
lililokuwa likimsumbua.
Pole Jide.
إرسال تعليق