
Vijana wenzangu na wasomaji wa makala. Hivi karibuni kuna vitendo
vimeanz kujijenga katika jamii yetu ambayo haviyoi ishara nzuri
tuendako.
Matukio ya kupigwa risasi padri na kuchomwa makanisa
na harakati za muamsho. Haya yote pamoja na yaliyotokea geita si mambo
ya kufumbiwa macho. Ninaomba niwasihi watanzania wenzangu kuwa haya si
mambo yanayoweza kutuimarisha katika
umoja na mshikamano wetu. Niwasihi tena kukumbuka kuwa umoja na
mshikamano wetu haukuja kama ajali ni misingi ambayo wazee na waasisi wa
nchi zetu walikubaliana na kuimarika katika mioyo yao, tusidharau na
wala tusibeze.
Mwisho nirudie kuwaomba nikiwakumbusha kauli ya
Raisi wetu wa jamhuri ya Muungano kuwa ".... Hivi ni vitendo ambavyo
sisi wenyewe tunavipanga. Ni jukumu letu viongozi wa dini,wanaharakati
na wanasiasa kukemea haya. Endapo tutaamua kukemea haya kwa vitendo
havitaendelea."
Poleni sana waumini wa dini kwa kupoteza
kiongozi wenu nami naungana nami katika kuomboleza na NINALAANI kitendo
hiki.
Vijana wenzangu na wasomaji wa makala. Hivi karibuni kuna vitendo vimeanz kujijenga katika jamii yetu ambayo haviyoi ishara nzuri tuendako.
Matukio ya kupigwa risasi padri na kuchomwa makanisa na harakati za muamsho. Haya yote pamoja na yaliyotokea geita si mambo ya kufumbiwa macho. Ninaomba niwasihi watanzania wenzangu kuwa haya si mambo yanayoweza kutuimarisha katika umoja na mshikamano wetu. Niwasihi tena kukumbuka kuwa umoja na mshikamano wetu haukuja kama ajali ni misingi ambayo wazee na waasisi wa nchi zetu walikubaliana na kuimarika katika mioyo yao, tusidharau na wala tusibeze.
Mwisho nirudie kuwaomba nikiwakumbusha kauli ya Raisi wetu wa jamhuri ya Muungano kuwa ".... Hivi ni vitendo ambavyo sisi wenyewe tunavipanga. Ni jukumu letu viongozi wa dini,wanaharakati na wanasiasa kukemea haya. Endapo tutaamua kukemea haya kwa vitendo havitaendelea."
Poleni sana waumini wa dini kwa kupoteza kiongozi wenu nami naungana nami katika kuomboleza na NINALAANI kitendo hiki.
إرسال تعليق