
.
Siku ya Wapendanao february 14
imekua nzuri kwa watu wengine na mbaya kwa watu wengine, kwanza kabisa
ni msiba wa msanii Goldie wa Nigeria ambae aliwahi kuiwakilisha nchi
hiyo kwenye shindano la BBA 2012, pili ni model aliyeuwawa kwa risasi
South Africa kwa kudaiwa kumfanyia mpenzi wake suprise lakini mpenzi
wake akajua ni jambazi, tatu ni mwigizaji Mtanzania Matumaini kukimbizwa
hospitali ghafla baada ya kuzidiwa.
Matumaini ambae anameza dawa 15
kila siku kutokana na matatizo ya miguu kuwaka moto, ini pamoja na figo
kumsumbua.. alipewa na Meya wa Ilala Jerry Silaa msaada wa gari la
wagonjwa lililotumwa mpaka kwao Vingunguti kwenda kumchukua baada ya
hali yake kuwa mbaya zaidi.
Kwa sasa amelazwa katika
hospitali ya Mnazi mmoja Dar es salaam ambapo mpaka jioni ya february 14
hali yake haikua nzuri, amekua akiishi Msumbiji kwa miaka mitatu baada
ya kuolewa na raia wa nchi hiyo, alikwenda huko kutafuta maisha baada ya
kufanya uamuzi wa kwenda kuuza kopi zake 300 za movie yake ya Comedy.

.

.

.

Baadhi ya waigizaji wa movie Tanzania waliojitokeza kwenda kumjulia hali.
إرسال تعليق