MAUAJI YA MAPADRI ZANZIBAR
Uchambuzi yakinifu kwa kuzingatia utaalamu wa makosa ya
jinai
1: UTANGULIZI
Watu wasiojulikana
walimpiga risasi kichwani Padri Ambros
Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar
siku ya Jumatano (boxing day) tarehe 26 Desemba 2012.Tukio hilo
lilitokea baada ya Askofu Michael Hafidh wa Kanisa la Anglikan Zanzibar kudai kuwa kumekuwepo vipeperushi vilivyosambazwa
vikiwatisha watu wenye imani ya Kikristo na kuiomba serikali iongeze ulinzi na kuimarisha
usalama. Kwa bahati, Padri Mkenda hakufa na anaendelea na matibabu.
Jumapili 17 Februari
2013, Padre mwingine wa Kanisa la Katoliki Zanzibar, parokia ya
Minara Miwili lililopo mji mkongwe, Padri Evarist Mushi amefariki dunia baada ya kupigwa Risasi utosini na watu wasiojulikana.
Padri huyo alikuwa akielekea kuendesha misa ya saa 3 asubuhi kwenye kanisa la Mt. Theresia
na akiwa eneo la Mtoni alisimamishwa na watu wawili ambapo mmoja wao alimpiga
risasi utosini na kufariki papo hapo.
Hili
ni tukio la pili kwa Mapadri kushambuliwa huko Zanzibar ndani ya kipindi
cha miezi miwili. Cha ajabu ,mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa hukusika na matukio
hayo.
2: Uchambuzi
wa Kijinai
Matukio
haya ni ya kupangwa na yanafanywa na serial killers na wahusika ni
walewale kwa sababu zifuatazo:-
1) Waliompiga
risasi kichwani Padri Mkenda tarehe 26 Desemba 2012 na waliompiga irsasi
klichwani Padri Mushi ni walewale kwa sababu matukioyote mawaili pikipiki aina
ya vespa imetumika.
2) Mauaji
yote yametokea katika eneo moja au maeneo ya jirani. Ni Zanzibar ileile…..na
wauaji hawaishi mbali na maeneo ambayo wamefanya matukio.
3) Mauaji
hufanyika wakati wa asubui.
4) Bila kubisha ni mauaji ya kidini.
5) Makanda
ya risasi katika tukio la Padri Mkenda na Padri Mushi yanaweza kuwa maganda ya
bastola ya aina moja.
6) Aina
ya uuaji …kwa kupiga risasi kichwani umefanyika katika matukio yote.
7) Kitendo
cha kumpiga mtu asiye na kosa (ambaye hawezi kujitetea) risasi kichwani ni
ushahidi kuwa wauaji walidhamiria kuuwa.
8) Mauaji
yote haya inaonesha kijinai yamepangwa kwa ustadi mkubwa kabisa. Wauaji ni
wawili ila wana watu wanaowaelekeza kuuwa nyuma yao.
9) Mauaji
yote hufanyika jumapili au siku ya ibada wakati mapadri huwa wanaenda kanisani
kwa sababu ni siku ambazo hakuna watu wengi katika maeneo husika.
10) Kwa
vile wanaolengwa ni mapadri ni vigumu kusema mauaji haya si ya kidini hasa
ikizingatiwa hali ya vujo za kidini ilivyo Zanzibar na nchini kwa ujumla.
11) Wauaji
hawa huitwa serial
killers kwa vile huuua mtu mmoja na kisha
kuendelea kuuwa watu wengi na iwapo hawatakamatwa huendelea kuuwa zaidi. Mfano wa watu hawa ni Ndugu
Carl Eugene Watts wa huko Texas, Marekani ambaye kati ya mwaka 1970
hadi 1982 alikuwa ameua watu zaidi ya 100 wote wakiwa wasichana/wanawake wadogo,
alipenda kuwaua nyakati za asubui kwa kuwanyonga na wengi wakiuliwa siku ya
jumapili. Muuaji huyu alipewa jina la utani ‘The Sunday Morning Slasher’…yaani
muuaji wa jumapili asubui.
12) Kwa vile wauaji ni wawili
kwa mujibu wa mashuhuda waliowaona basi mauaji haya hupangwa na pia hugawana
majukumu.
13) Pia kuna uwezekana kuwa
wauaji hushirikisha watu wengine ambao huja eneo la tukio kuangalia hali ya
usalama na vilevile wauaji hawa huwasiliana kwa simu kujua muda ambao
wanayetaka kumuua huwa yupo nje ya nyumba yake au barabara.
14) Wauaji hushirikiana na
wahalifu wengine wanaokuwa jirani na eneo la tukio ili kujikinga.
15) Kabla ya mauaji kutendeka
wauaji hawa hufanya mikutano uso kwa uso, huwasiliana kwa njia ya simu, pia
hutumia lugha maalum ambayo ni ya kwao tu, hukusanya taarifa za watu wa kuwaua,
wana viongozi wao wanaowaelekeza na wana watu wanaowasaidia.
16) Lengo
la wauaji hawa ni kuuwa. Padri Mkenda alisalimika kwa bahati tu. Lakini
akijaribu kurudi Zanzibar lazima atamaliziwa kwani wauaji hufurahi wanapoua na
kuumua mtu ambaye walishindwa kumuua ni furaha kwao.
17) Baada
ya kushindwa kumuuwa Padri Mkenda ; wauaji walipanga wasikosee katika
kumuua Padri Mushi ndio maana risasi iliengwa vizuri utosini kuhakikisha
anakufa papohapo.
3: Tabia za wauaji wa mapadri wa Zanzibar
Ukiangalia
jinsi mapadri hawa wa Zanzibar
walivyopigwa risasi utagundua kuwa wasifu na saikolijia ya jinai ya wauaji hawa
ni zifuatazo:-
1) Wauaji
umri wao ni kati ya miaka 19 na 46, wanaume, ngumu kwao kupata kazi za maana,
wana matatizo ya kisaikolojia na wana imani kali ya dini yao. Wauaji hawa hata kama
wana ajira ni vigumu kukaa na ajira moja kwa muda mrefu.
2) Wauaji
wote ni waumini wa dini moja ndio maana hulenga victims wao kutoka dini nyingine.
3) Wauaji
ni watu ambao hawana kazi za kudumu.
4) Wauaji
ni watu ambao maisha yao ya utotoni hayakuwa
mazuri sana.
5) Wauaji
ni watu ambao hawakufanya vizuri shuleni na darasani.
6) Wauaji
ni watu ambao misingi yao
ya maisha inayumba.
7) Wauaji
ni wabinafsi, wabaguzi wa kidini, hawana huruma, wana penda kusifiwa na
wanapenda kujipendelea.
8) Mpango
wa siri wa wauaji hawa ni kuuwa mapadri au waumini wa dhehebu fulani lakini
hasa mapadri.
9) Wauaji
hawa wasipokamatwa wataendelea kuuwa mapadri.
10) Hakuna mtu atakaye weza wazuia kuuwa mapadri
labda tu wakikamatwa na dola.
11) Kwa
hali fulani inaonesha wauaji wana elimu ndogo sana ya masuala ya kidunia.
12) Wauaji ni wapenzi wa vyombo vya habari na
hupenda kusoma na kutunza magazeti hasa yanayohusu matukio ya mauaji/uhalifu wanayoyafanya.
13) Wauaji
hawaui kwa ajili ya kutafuta pesa au mali bali wanaua ili wapate
umaarufu kwa wanaowatuma (attention
seekers).
14) Wauaji
ni watu wenye kipato cha kawaida, kati au chini kabisa.
15) Wauaji
wanaamini wanaua kwa sababu ya dini na hivyo hawana kosa wala hatia.Jambo
ambalo si sahihi. Huko Uingereza mwaka 1993, msichana mwenye miaka 17, Shafilea Iftikhar Ahmed aliuwawa na
wazazi wake kwa vile alionekana hafuati masharti ya dini za wazazi wake. Wazazi
wake waliamini kuwa kuuwa ili kulinda imani ya dini ni jambo sahihi.
16) Wauaji
ni wafuasi ambao wamefundishwa kuwa dini nyingine ni adui jambo ambalo si
sahihi.Wanasahau kuwa vitu vingi vinanyowazinguka na wanavyovitumia pia huwa
vimetengenezwa na watu wa dini nyingine. Mfano wauaji wanatumia pikipiki za vespa scooter ambazo hutengenezwa na
nchi ambayo si ya kidini. Vespa ni neno la kiitaliano lenye maana ya wasp yaani mdudu arukaye jamii ya nyuki.
4: Mifano ya mauaji kama
hayo hapa duniani
Dr.
Harold Fredrick Shipman wa Uingereza ni moja wapo wa serial killer dunia iliwai
kumpata. Kati ya mwaka 1974 hadi 1998 aliuwa watu aidi ya 250 huko Uingereza.
Wengi wa aliwaua walikuwa wagonjwa wake wazee na watu wenye umri mkubwa. Wengi
wa aliowaua walikuwa wanawake. Mtu mwenye umri mdogo aliyemuua alikuwa na miaka
41. Dr. Shipman, tofauti na wauaji wa Zanzibar
wanaotumia risasi, Dr. Shipman alikuwa akiuwa wagonjwa wake kwa kutumia diamorphine na pethidine. Pia yeye
mwenyewe ndiye aliyekuwa anaandika katika vyeti vyao vya vifo sababu za vifo
vyao.
Dunia
iliishapata serial killers ambao huwa
wanauwa watoto tu, wanawake peke yao, washoga
peke yao, wanaume peke yao,
rangi fulani peke yao, makahaba peke yao n.k. Mauaji haya nia
anina mpya nyingine ya mauaji.
5: Ushauri
kwa polisi
Polisi
na wapelelezi wanapaswa wajue aina ya vespa
iliyotumika, rangi yake, aina ya matairi, alama za matairi, rangi ya nguo za
wauaji, wajihi na sura za wauaji kwa kusikiliza maelezo ya mashahidi
walioshuhudia mauaji, namba za usajiri za vespa
hiyo hata kama walioshudia walikariri namba
moja tu. Si lazima wakariri namba zote.
Ni
vema polisi waandae mtego mwingine wa kuwakamata wauaji kwani watarudia tena
kuuwa ndani ya siku 30 hadi 120 kutoka tukio la hivi karibuni. Si sahihi kwa
polisi kupeleleza bila kuandaa mtego makini.
Polisi
hawawezi kushughulikia suala hili kwa umakini kwani hata katika nchi
zilizoendelea kama Uingereza na Marekani;
polisi hawakufaulu hadi wataalamu wa makosa ya jinai waliposhirikishwa. Anaweza
kujitolea kuwasaidia polisi katika upelelezi kama
wataitaji msaada wangu. Hatua za haraka
zisipochukuliwa mapema hali itakuwa mbaya zaidi.
NB mwandishi wa uchambuzi huu ni mwanasheria jijini Dar es salaam
Post a Comment