Mastaa wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Steven
Mengere ‘Steve Nyerere’ wanadaiwa kuwa kwenye bifu zito kisa kikielezwa kuwa ni
mwigizaji , Ruth Suka ‘Mainda’,
Inadaiwa kuwa chanzo cha yote ni pale Steve Nyerere
alipoanzisha kampuni ya kazi zake za sanaa akimshirikisha Mainda, jambo
linalosemekana kumkera Ray aliyekuwa akifanya kazi na mwigizaji huyo wa kike
chini ya Kampuni ya RJ Production.
“Kuna wakati eti Ray huwa hapendi kumuona mtu akiwa karibu
na Mainda, mara nyingi huwa anakuwa na wivu kwa kuwa anahisi kuna kitu zaidi ya
kazi,” kilisema chanzo kingine na kusisitiza kuwa Ray alimpiga ‘stop’ Mainda
kushirikiana na Steve Nyerere huku suala la wivu wa kimapenzi likitajwa.
Ilidaiwa kuwa kabla ya mtafaruku huo, Steve Nyerere na Ray
walikuwa ni maswahiba lakini sasa wamegeuka chui na paka na katika kutafuta
‘sosi’ ya yote hayo, ndipo Mainda akatajwa.
Baada ya taarifa hizi kusambaa wasanii hawa walitafutwa alipatikana
Steve Nyerere lakin kwa Upande wa Ray alikosekana kwenye simu yake ya kiganjani
na pia kwa upande wa mainda simu yake iliita lakin hakupokelewa
Steve
Nyerere alisema hivi
“Ni kweli
mimi na Ray ni chui na paka lakini sitaweza kukwambia sababu ya ugomvi wetu kwa
kuwa nitaibua mambo mengi sana, kipindi hiki nipo katika kubadilisha maisha
yangu,”
Post a Comment