Serikali
ya Gambia imetambulisha mfumo mpya wa siku za kufanya kazi kwa
wafanyakazi wa serikali ambapo sasa watafanyakazi kwa siku nne tu, huku
siku ya Ijumaa nayo ikiwa siku ya mapumziko.
Rais
wa nchi hiyo Yahya Jammeh (pichani) amesema wananchi wa Gambia ambao
wengi wao ni waislamu sasa watapata muda zaidi kusali, kushiriki
shughuli za kijamii na kulima mashamba yao.
Kwa
mujibu wa taarifa ni kuwa sasa wananchi wa Gambia wanapaswa kuingia
mashambani kupanda mazao ya chakula na kutumia chakula hicho ili taifa
hilo liwe tajiri.
Rais
huyo amesema mishahara haitapunguzwa kwa sababu kwa siku hizo nne watu
watafanyakazi zaidi ya saa za kawaida ili kufidia siku ya tano.
Shule
za serikali sasa hazitafunguliwa tena Ijumaa, ila sekta binafsi
zitafanyakazi zao ila hazitaweza kufanya biashara yeyote na serikali
siku hiyo.
Rais Jammeh mwenye historia ya kuwa na tabia za kustaajabisha hajawapa wananchi wa Gambia muda wa kujiandaa kwa mfumo huo mpya.
Rais Jammeh aliingia madarakani kwa mapinduzi yaliyomwaga damu mwaka 1994.
MO BLOG: Gambia
imepunguza siku za kufanya kazi kwa wafanyakazi wa Serikali bila
kuwapunguzia mshahara kwa lengo la kuongeza ufanisi ili wapate muda wa
kusali na kwenda mashambani kufanya shughuli za Kilimo…Ndugu zangu
utaratibu kama huu utakapokuja Bongo siku za kufanya kazi 4 yani J3
Mpaka Alhamis mshahara ulele…nyumba za Ibada na mashambani ataonekana
mtu…??
إرسال تعليق