Umoja wa Mataifa nchini Sudan
unasema mauaji ya watu zaidi ya 50 yaliyotokea Jumamosi kaskazini mwa
Darfur ni pigo jengine dhidi ya juhudi zake za kusambaza msaada kwa
maelfu ya watu waliokimbia ghasia za kikabila za hivi karibuni.
Inakisiwa kuwa watu kama laki moja wamekimbia makwao katika jimbo la Darfur Kaskazini tangu awali mwezi wa Januari wakati ghasia zilipozuka kuhusu haki ya kuchimba madini baina ya makundi ya Waarabu yanayozozana.
Juma hili inatimia miaka 10 tangu vita vya Darfur kuanza.
Watu karibu milioni moja na nusu wa Darfur wanaishi kwenye makambi ya wakimbizi.
Post a Comment