
Maandamano nchini Tunisia baada ya mauaji ya mwanasiasa wa upinzani Chokri Belaid
Waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebali, amejiuzulu baada ya kukosa kuafikia makubaliano kuhusu serikali mpya.
Bwana Jebali,alikuwa anajaribu kuunda serikali
mpya kufuatia msukosuko wa kisiasa uliosababishwa na mauaji ya
mwanasiasa wa upinzani Chokri Belaid wiki mbili zilizopita.
Awali alisema alikuwa tayari
kujiuzulu ikiwa chama chake cha kiisilamu cha Ennahda hakingeunga mkono
mpango wake wa kuwateua wataalamu kama wanachama wa baraza la mawaziri.
Mauaji ya mwanasiasa huyo yaliyofanyika Februari
sita, yalisababisha maandamano na ghasia pamoja na kujiuzulu kwa
maafisa wa serikali.
''Niliapa kuwa ikiwa mpango wangu haungefaulu,
ningejiuzulu, na nimefanya hivyo,'' alisema bwana Jebali baada ya
kukutana na rais Moncef Marzouki.
Akitaja hatua yake kama jambo la kusikitisha , alisema aliamua kujiuzulu ili kutimiza ahadi yake kwa wananchi wa Tunisia.
"watu wetu wana ndoto fulani, ambazo wanataka
wanasiasa kuwatimizia. Laizima tuweze kuwaweka imani watu wetu,''
alisisitiza Jebali.
Na aliongeza kuwa, kukosa kufaulu kwa mpango
wangu, haina maana kuwa Tunisia imefeli, au mapinduzi hayakuwa na
faida,'' akigusia mapinduzi ya kiraia yaliyofanyika miaka miwili
iliyopita ambapo rais wa zamani Zine al-Abidine Ben Ali alipinduliwa.
- BBC
Post a Comment