Ukingoni mwa Ziwa Tanganyika- picha ya Revocatus Meza, Desemba 2012. Wimbi la “blogging” liliikumba dunia kati ya 1995 hadi 1998 na kuanza kumea kwetu Tanzania kupitia mwanahabari Ndesanjo Macha
miaka kumi iliyopita. Wakati Ndesanjo anaanza kublogu si wengi
tuliomwelewa. Nakumbuka alivyokua akiniongelea juu ya fani hii kwa
hamasa kwenye 2002. Baadaye kidogo aliendesha Jikomboe, blogu lililokua na taswira ya majani mabichi ya ukoka. Enzi hizo hakukua na hata senti moja aliyoichuma.
Ndesanjo Macha- mwasisi wa blogu Tanzania
Ndesanjo alikua akisema blogu ni dunia ya kesho ya mawasiliano. Wakati
huo vyombo vikubwa vya habari nchi zilizoendelea vilianza kuona umuhimu
wa blogu vikaanza kuunda idara pembezoni mwa tovuti zake mama. Kwetu
wenye magazeti wengi hawakupenda wanablogu;waliwaona washindani. Mwaka
ambapo wanablogu wetu walianza kuchomoza ilikua 2006 baada ya kifo cha
wapenzi wawili wa Kitanzania waliouliwa kinyama Marekani. Blogu la Michuzi (ambalo halikua maarufu kama leo) na Radio Butiama
(inayojulikana kwa jina Podcast) zilisimama dede kutangaza habari hizo.
Hapo ndipo miye binafsi nilipoanza kuona namna wanablogu walivyokuwa na
mwendo mkali - zaidi ya vyombo vya habari vya kijadi. Niliingia rasmi
uwanjani mwaka 2007- nikisaidiwa na Ndesanjo na wanabloga wengine
walionitangulia; akina Simon Kitururu, Jeff Msangi (Bongo Celebrity)
mathalan. Nilichogundua siku za mwanzo ni kwamba Blogaz husaidiana
sana. “Ukiwa mbinafsi huendelei kama Bloga” alisisitiza Ndesanjo.
Mbuzi wetu Bongo
wakila kila aina ya takataka mitaani. Nyama yake tamu. Lakini je, ina
nini kinachotudhuru tusichokijua? Nilipiga picha hii, Zanzibar, mwaka
2011. Leo Jikomboe na ule ukoka havipo tena. Ndesanjo, mwasisi wa blog za Kiswahili duniani, anafanya kazi shirika la habari- Global Voices.
Kati ya mamia ya waandishi wa shirika hilo la kimataifa, Mtanzania huyu
anaongoza kwa habari asilia za uchambuzi zaidi ya 4,200 . Tofauti ya
mtu kama Ndesanjo na baadhi ya blogaz ni kwamba yeye kiasilia ni
mwanahabari hivyo anachanganya ujuzi na mitindo hii miwili ya kusanifu
matukio. Si ajabu mwaka jana Ndesanjo alishinda tuzo la Mwanablog bora
wa Afrika.

Lugha
ya blogaz na vyombo asilia vya habari zi tofauti. Wanahabari lakini ni
watu waliosemea sawasawa kazi zao na kufuata utaratibu wa lugha,
kusahihisha na kuhariri kazi. Bloga ni mtu yeyote tu mitaani au kijijini
anayetaka kuelezea jambo.
Samaki aitwaye Kuhe katika Ziwa Tanganyika. Picha nimeletewa na mwandishi Revocatus Meza.
Mvua ya blogaz Tanzania imejaza bahari safi tena ya faraja. Blogaz ni
wengi tena wa kila rangi na jinsia; wanatupasha matukio kila sekunde!
Wakati tukianza, wanawake hawakua wengi. Mwaka jana mshindi wa Blogaz
bora Bongo alikuwa Mwanamke na Nyumba. Nyingine zimekuwa makutano au baraza la maoni na malumbano muhimu- mfano Jamii Forums, iliyoundwa 2006. Zipo zenye mafunzo mazito- angalia Al Hidaaya
inayofunza masuala ya Kiislamu na Korani tutaelewana n’na maana gani.
Zile zenye kurasa moja (kama zangu) zimegeuzwa viwanda vidogo; mathalan
ya Maggid Mjengwa ambayo ni kijigazeti cha ajira. Ajira
zinazowahudumia na kuwafariji wanahabari wake. Mara nyingine zina maudhi
maana hata kuzifungua zinakua shida maana matangazo yamejazana pale juu
kiasi ambacho si tena habari bali duka. Ama kweli mtandao umekuwa
biashara. Uzuri upo ndiyo; ubaya tuuseme pia!
Msukuma mikokoteni akitotwa jasho saa za alasiri, mitaa ya Magomeni Mapipa. Niliipiga picha hii mwaka 2009, Dar es Salaam.
Watanzania tunakwenda na wakati si uongo. Maana ukitazama wenzetu nchi
zilizoendelea wanaelekeza kila jicho katika mtandao na inteneti. Maduka
makubwa makubwa asilia nchi magharibi yanapata hasara na kufunga virago
vyake. Mwishoni mwa mwaka jana asilimia 25 ya biashara zote nchi
zilizoendelea zilitokana na makampuni yenye mauzo ya mitandaoni –
yakaingiza dola bilioni 1.7! Linaloongoza sasa hivi ni Amazon
inayouza kila kitu bei rahisi na kwa ufanisi zaidi kuliko maduka asilia.
Makisio ya faida ya Amazon mwaka jana yalikuwa dola bilioni 63.
Uingereza duka maarufu la muziki, sinema na vitabu- HMV-
lilipunguza wafanyakazi mwezi jana na tetesi ni kuwa wameshafifia
kibiashara. Ama kweli mtandao ndiyo soko mzazi wa biashara leo na kesho
(kama alivyosema Ndesanjo) na wanabloga wetu wanakwenda na wakati.
Mwandishi gwiji wa Kiswahili Ebrahim Hussenaliwahi kuandika
“wakati ukuta ukipigana nao utaumia.” Ndiyo maana wafanya biashara
wanatangaza bidhaa kupitia blogu. Ndiyo hali halisi ilivyo.
Kitabu kipya cha Prof Said Ahmed[/caption]
Kitabu kipya cha Mwandishi nguli, Profesa Said Ahmed- Mhanga Nafsi Yangu- ambacho kinamwangalia mwanamke wa Kibongo anayekwenda kusoma ughaibuni. Kimetolewa na Sasa Sema (Longhorn) wa Kenya,2012.
Ila tutathmini zaidi hilo... Blogu zilibuniwa kutangaza mambo na kadhia
ambazo hazipo ndani ya vyombo habari mama na runinga. Zilibuniwa
kumfaidisha mwananchi yeyote wa kawaida akibeba kamera na simu yake
mkononi akaeleza habari za pale anapoishi. Hicho ndicho chanzo... Kama
hukua na nafasi kuna Twitter ambayo ni fupi zaidi (maneno 30
tu!). Zana hizi ni muhimu sana kwa jamii ya leo. Hizi ni “habari za raia
wa kawaida” . Umuhimu wa Blog, Twitter na You Tube umeonekana
pale yalipotokea machafuko na harakati mbalimbali duniani kama Tunisia,
Misri, Libya na Mashariki ya Kati nzima miaka miwili iliyopita. Dhoruba
za mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi zilisambaa dunia nzima haraka
kutokana na uwezo huu muadhama. Nguzo zake ndizo hizo. Google
ambaye hulipa matangazo ya biashara kutokana na “maudhui ya habari”
husisitiza wanablogu na waandishi kuwa wa kweli na kutochezea kazi za
wenzao. Kwetu Bongo hapana. Miaka ya karibuni makampuni makubwa makubwa
na mabenki kama National Microfinance (NMB) yanasaidia kuwekezea
wajisiria mali wadogo wadogo (yaani Blogaz). Mara nyingi makampuni haya
hayaangalii kama wanablog hawa wananukuu kazi za wenzao, wanaandika
mambo yao wenyewe au wanakopi tu na kubandika.
Nembo ya kutetea haki za wanyama pori wanaouliwa ovyo. Kampeni hii inaongozwa na Kidon Mkuu Ngoille Mkuu, wa Arusha.
Dili zinapatikana kwa kujuana juana, mathalan. Bahati mbaya kumezuka
mtindo wa wanablogu wengi kutwaa kazi na picha za wenzao bila kuandika
zimetoka wapi. Ukilinganisha sasa hivi Blogu zetu Tanzania ni tofauti
sana na za nchi nyingine maana wengi hatuandiki vitu tulivyovibuni au
tunavyoviona. Mmoja akishaandika tu basi wengine wote tunakopi na
kubandika tu bila kuangalia sana kazi ikoje. Siku Google na mashirika
miliki ya hizi blogu wakifahamu yatakua mengine. Kwa sasa tunajificha
ficha tu.
Mwanamichezo na mwanahabari Israel Saria akiwa kazini na vijana Dodoma miaka ile ya Themanini. Niliongea na Israel Saria, anayeendesha blogu-tovuti la Michezo Tanzania (Tanzania Sports)
tokea London karibuni. Saria ameendesha shughuli hii toka 2005 na
anafadhiliwa na NMB. Mbali ya kuwa mtangazaji wa michezo BBC, Saria ni
mwalimu rasmi wa mchezo wa mpira wa nyavu aliyekuwa kocha miaka mingi
Tanzania. Alipendekeza wawekezaji kuangalia thamani ya blog mbalimbali
kabla ya kuzipachikia matangazo: “Hebu linganisha blogu zetu na za
majirani wa Kenya. Wakenya wengi huandika mambo wanayobuni. Sisi
tunakosa ubunifu na uhalisia. Mwenzetu akiandika habari- baada ya dakika
tano –mabloga wengine wote tunainukuu na kuitangaza ikiwa imejazana
makosa. Tunalipua tu. Hatuna hata muda wa kuichunguza au kuihariri.
Tunadhani kublogu ni suala la umaarufu na kuonekana kwamba na mimi nipo;
eti sitaki nionekane kwamba nimekosa ile habari iliyotangazwa na
mwenzangu!” Saria anaongeza kusema kwamba wengi wetu tunashindwa
kutambua kwamba Google huwa wanajua na kuangalia kazi asilia.
“Ukishatundika tu kazi yako, baada ya dakika chache tayari inasajiliwa
kama ni mali yako. Yeyote anayeinukuu au kuitumia hatambuliwi kama
mwenye hiyo kazi.” Mabloga wengi Bongo basi wanarudia rudia tu kazi za
wenzao kwa kuzitapika na kuzitafuna kama ambavyo ng’ombe wanavyofanya
baada ya kula majani. Matokeo baadhi ya blogu leo zimegeuka mabango ya
matangazo badala ya kazi muhimu za kifasihi. Zipo blogu nyingi
zinazobuni mambo- lakini pia zipo ambazo zinacheza tu.
Picha ya Maandazi toka tovuti la Taste of Tanzania. Picha ya Miriam Rose Kinunda... Miriam Rose Kinunda anayeendesha tovuti-blogu ya mapishi (Taste of Tanzania)
amekuwa akisanifu blogu na kusaidia wenzake kuzijenga toka 2004.
Anasema ni mara nyingi sana ambapo kazi na picha zake zimetumiwa bila
idhini. “Awali nilikua nikiblogu Kiswahili na Kiingereza, lakini
kutokana na huu wizi wa kazi, nimeondoa kabisa kitengo cha Kiswahili
nikabakisha Kiingereza kwa wasomaji wa kimataifa.” Miriam ambaye
karibuni atatoka na kitabu chake cha mapishi anataja mfano ambapo tovuti
moja maarufu ya Kenya iliiba kazi na picha zake. Akaamua kuwapigia
simu. “Baada tu ya dakika tano, jamaa walinitumia barua pepe kunitaka
radhi. Walionyesha namna walivyo waungwana.”

Miriam Rose Kinunda
Je nini kifanyike? Saria na Bi Kinunda wanashauri wawekezaji (mathalan
benki inayowafariji wanablogu kama NMB) kufadhili na kusaidia tu wale
wanaokua wabunifu na wanaofuata kanuni za fani hii muhimu katika jamii.
Kigoda
nyumbani kwa mpigania utamaduni wetu na mfanyabiashara mashuhuri wa Dar
es Salaam, Mwafrika Merinyo anayeendesha shughuli za Afrika Sana. Nilipiga picha Novemba 2011. Makala hii iliandikwa pia kwa Kiingereza katika safu ya Mwandishi gazeti la Citizen mwezi jana

إرسال تعليق