YAMOYONI:Shindano la mkali wa rhimes kama lingefanyika mwaka 2012 au
2013 nadhani tungesema Afande sele amechinja kondoo 100 wa kafara ili
ashinde ama ameua albino,kipindi kile Juma nature anatamba na album yake
ya ugali ,Ferooz na nyimbo yake ya ukimwi,Professor,Dully & Mr Nice
kipindi kile wanaonekana miungu watu nadhani ingekua kile kizazi ni
kizazi kama tulichonacho sisi kwasasa ungesikia hawa ni
mafremason,mwingine angesema hawa ni wachawi wanatembelea nyota za akina
Ngurumo,jumbe,shaban dede ama mzee issa matona.Lakini kuonesha tofauti
ilokuepo kati ya kizazi kile na hiki wale walikua wamekaa kimya kila mtu
akijaribu kutafuta njia ya kupata mashabiki kupitia staili mbalimbali
za kimziki.Amini ninachokwambia kuna tofauti kubwa sana kati ya kizazi
kile cha mziki ule na kizazi hiki cha sasa cha kina Bob jr na Ney
wamitego,na ndomana kikaitwa kizazi kipya na upya umedhihirika.Sasa
nirudi kwenye mada yangu.Kwamimi ninachofahamu ni kwamba mganga ndo siku
zote atakaekwambia nani anakuroga,na unapomsikia mtu anasema karogwa
ujue alienda kwa mganga sasa jiulize alifuata nini?Hapa tunapause
kwanza...... Hili suala la mtu anakurupuka na anamtaja msanii mwenzake
anamroga yeye amejuaje? kama hajaenda kwa mganga?Hapa unagundua ule
ubunifu wa AY kufanya commercial,Dully na mwanasesere ama TMK kufanya
Rap katuni wasanii wasasa wamekosa na ndomana wanatafuta mbinu mbadala
ya wao kujulikana. Nategemea nione wasanii wakitumia mda huu kuandika
nyimbo kali ili watanzania wawaelewe na pia wafanye video nzuri ili
wavuke boda lakini bado baadhi yao hawafanyi mazuri yakuwasaidia bali
wanajenga malumbano na maneno yasiojenga mziki wetu.USHAURI wangu kwa
wasanii ni wawe na uvumilivu,waheshimiane na wafanye kazi ili sisi
mashabiki tufurahi na tuelimike pia.Tukumbuke pia mziki ni ajira kwa
watu wengi sio wenye vipaji vya kuimba na producers tuu,tujue kua kuna
kuzaliwa na kuna kufa,binadamu sote sawa tumeumbwa kwa mfano wa yeye
tunaemuamini haya ya duniani yakupita tu tuyaache yapite sisi tupendane
maisha yaendelee.yangu yalikua hayo tuu kwa leo nawatakia kazi njema
ndugu WANDEWA STREET 4 LIFE c.e.o ally stly
Yaliyo Moyoni Mwangu Kuhusu Wasanii wa Bongo Flava Kusingiziana Uchawi
Hisia
0
Tags
ENTERTAINMENT
إرسال تعليق