""Napenda kuwapa taharifa Mashabiki wangu Wapenzi wa Muziki wangu na
Ndugu Zangu wenye mapenzi Na Muziki wangu kuwa naskitika na naskia
uchungu Sana Kwa kampuni ya sim Tigo kwa kuuza Kazi yangu ya "Kuwa Na
Subira"toka mwaka jana mwezi wa 6 Bila makubaliano na Muhusika mkuu
ambaye ni Mimi Rama Dee tafadhari ndugu zangu naomba mnisaidie sitaki
kupita njia nyingine zaidi ya hii kuweka ukweli hapa..naumia sana sana
kuona Tigo inanikandamiza inafananya biashara Ambayo sio halali,najuwa
ndani ya Wapenzi wa Muziki wangu kuna Wansheria na Waandishi wa Habari
pia wapo watu wenye Blogs na Web naomba mnisaidie kuwajulisha wananchi
juu ya Manyanyaso ya Kampuni hii ya simu Tigo Hii inaonyesha ni jinsi
Gani hakuna haki wala heshima kwenye sanaa,pia kutumia njia ambayo
haitambuliki kuwadanganya Wananchi kuwa hiyo ni kazi halali ambayo
imetoka kwangu..Ndugu zangu Tigo wanaharibu Mahusiano yangu na Nyie
Mashabiki wangu Kwa maana wanauza kazi kwa njia sio halali...Kama
umenunuwa Kazi yangu Ya Kuwa Na subira Tigo basi juwa wamekudhurumu haki
yako ambayo ilikusudia kunichangia mimi.""
ALICHOKIANDIKA RAMA DEE KUHUSU KUIBIWA KAZI YAKE NA KAMPUNI YA TIGO
Hisia
0
Tags
ENTERTAINMENT
إرسال تعليق