Katikati ya juma hili blogu ya shaffihdauda.com
iliripoti tafiti inayo onyesha namna azam fc wanavyo tenda dhulma kwa
vilabu vingine vya ligi kuu ya vodacom vilivyo fika katika uwanja wa
Azam uliopo Chamanzi kupitia matangazo ya moja kwa moja kupitia luninga
ya star tv.
Uongozi wa azam fc wamekana tafiti hiyo iliyowekwa katika blogu ya shaffihdauda.com ikiwa na anuwani www.shaffihdauda.com/2013/03/madudu-ya-ligi-kuu-mechi-zinaonyeshwa.html
"Mechi
za VPL zinaooneshwa kwa udhamini wa SSB zimekuwa za dhuluma kuwa ni
uongo na uzushi," ilieleza taarifa iliyowekwa na meneja wa Azam fc
Patrick Kahemele katika ukurasa wa azam ndani ya facebook.
Kahemele
alieleza kuwa JKT Ruvu inayohusishwa katika tafiti hiyo na kudai kuwa
haijalipwa, anasema kuwa teyari wameshailipa na wako mbioni kuwalipa
Polisi morogoro.
"Klabu ya JKT Ruvu iliyotajwa kuwa imelalamika
ilipokea malipo toka kwa star tv yaliyolipwa na azam fc kwa niaba yake,
pia malipo ya Polisi moro yanaandaliwa na yatafanyika wiki ijayo,"
ilieleza taarifa ya Kahemele.
Kahemele alihitimisha taarifa yake kwa kuwaomba wananchi waipuuze tafiti hiyo;
"Tunawaomba wananchi waipuuze habari hiyo kwa kuwa ni uzushi".
"Tunawaomba wananchi waipuuze habari hiyo kwa kuwa ni uzushi".
إرسال تعليق