MWIGIZAJI
Nyota katika tasnia ya filamu Hapa nchini Tanzania Wastara Juma ‘Stara’
amesema kuwa baada ya muda mwingi wa mihangaiko ya kuuguza na hata
kumpoteza mumewe anahitaji kupata muda wa kupumzika na kujenga akili
upya, katika kulifanya hilo ameamua kwenda kupumzika Uarabuni kwa ajili
ya kutuliza akili na kujipanga upya,na jinsi gani ya kuendelea na
shughuli zake za uigizaji.
Wastara amesema “Nina safari wiki ijayo na kwenda Uarabuni kwa ajili ya kupumzika kisha baadae kuangalia nafanyaje kazi katika staili ipi, kwa sasa itakuwa ngumu kuwepo bila kufanya kazi lakini pia familia imeamua niende huko kama ni sehemu ya kunifariji zaidi kutokana na kipindi hiki kigumu,”anasema Stara.

![]() |
| Wastara pamoja na mtoto wake. |
Lakini mwanadada huyo asiye na makuu ameamua kwenda huko kupmzika kutokana na hali ya filamu ilivyo sasa ambapo watayarishaji wanajikuta wakikikaa kwa muda mrefu wakisotea kazi zao kutoka pasipo na wakati maalum, soko la filamu kwa sasa inasemekana ni gumu kuliko ambavyo jamii inaliona ukiona kazi imetoka sokoni ujue watu wametabika kwa kiwango kikubwa.

إرسال تعليق