
Msanii Ben Pol amesema kuwa ni wakati wa
kampuni zinazofanya biashara ya miito ya simu ya nyimbo za wasanii wa
muziki wa hapa nyumbani kuacha kufikiria kuwa wasanii siku hizi
hawajitambui.
Ben Pol alisema pamoja na kwamba yeye ni moja ya
wasanii ambaye ana nyimbo zinazotamba kama 'Pete', 'Samboira', 'Number
one fan', 'Nikikupata', lakini mpaka leo hana takwimu ya watu ambao
wamenunua kazi zake.
Anasema kuwa hivi sasa wasanii wanasoma na wana
taaluma zao wanajua wanafanya nini kwenye muziki na si kwamba mtu hana
kazi ndo kwa maana anafanya muziki.
Alisema pia ni vizuri serikali ikaingilia suala hilo ili wasanii wapate haki yao.
Alisema pia ni vizuri serikali ikaingilia suala hilo ili wasanii wapate haki yao.
Post a Comment