Chuo kikuu cha Somaliland chawezesha upatikanaji wa vitabu vya kiada

Chuo kikuu cha Gollis kimefungua maktaba ya kieletroniki yenye vituo 30 vya kompyuta tarehe 12 Februari. [Barkhad Dahir/Sabahi]
Na Barkhad Dahir, Hargeisa

Fatima Mohamed, mwenye umri wa miaka 24 mwanafunzi wa tiba katika chuo kikuu cha Gollis huko Hargeisa, hana haja ya kuendelea kuwa na wasiwasi tena kuhusu namna ya kupata nakala za vitabu vya kiada katika uga wake.

Vitabu vya kiada vimekuwa vikipatika kwa uchache nchini Somalia kutoka vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini sasa Mohamed ana nafasi nzuri ya kufikia vitabu kwa kupitia njia ya maktaba ya kieletroniki ambayo ilifunguliwa mwezi uliopita katika kampasi inayoendeshwa kibinafsi.

"Nina furaha kuhusu huduma hii kwa sababu itasaidia kuinua na kuimarisha maarifa ya wanafunzi ... imefanya kujifunza kuwa rahisi kwangu mimi," aliiambia Sabahi.

Maktaba ya vitabu vya kielektroniki ilikuwa ya kwanza ya aina yake kufunguliwa Somalia wakati wakuu wa Chuo Kikuu cha Gollis kilipoitangaza rasmi katika kampasi ya Hargeisa tarehe 12 Februari. Sasa wanafunzi wanaweza kukaa kwenye sehemu ya kufanyia kazi ya kompyuta na kupata vitabu kwenye skrini mbele yao.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Gollis waksoma kwenye maktaba ya kieletroniki iliyofunguliwa hivi karibuni, maktaba ya aina hiyo ni ya kwanza nchini Somalia. [Barkhad Dahir/Sabahi]

Aidaros Mohamed Abib, mkuu wa taaluma wa chuo kikuu, alisema maktaba ya kielekroniki ni bure kwa wanafunzi wa chuo kikuu 3,500.

"Kwa wakati mmoja, wanafunzi 30 wanaweza kukaa pale, kuwa na uwezo wa kutumia vitabu vinavyotumiwa na idara tofauti za chuo -- vilivyo vingi ni vitabu vya uhandisi, sayansi, udaktari, utawala na uongozi," Abib alisema.

Abib alisema anatumaini chuo kikuu kitaweza kuongeza idadi ya kompyuta katika maktaba ili kutosheleza wanafunzi wengi zaidi kwa wakati mmoja.

Zaidi ya hayo, mwezi ujao Chuo Kikuu cha Gollis kinapanga kuzindua sehemu ya mtandao, ambapo wanafunzi na wasio wanafunzi kwa pamoja wanaweza kulipa ada ndogo ili kupata vitabu kutoka katika eneo lolote kupitia intaneti.

"Tutaanzisha utaratibu [katika mtandao] utakaoweza kupatikana kutoka kokote, na kutoa uanachama kwa yeyote ambaye anavutiwa," alisema Walid Mohamed Ali, mkurugenzi wa idara ya teknolojia ya habari katika chuo kikuu.

Mara utaratibu huo utakapokuwa tayari kufanya kazi, utawawezesha watu kuvipata vitabu 50,000 vya ngazi ya chuo pamoja na mihadhara 10,000 ya video na ya sauti kwa njia ya mtandao, aliiambia Sabahi. Vitabu vingi vimechapishwa kwa Kiingereza, lakini baadhi vitapatikana kwa Kiarabu.

Kuanzisha maktaba ya kielektroniki kutasaidia kutatua tatizo la ukosefu wa vitabu vya kiada na vya ziada huko Somaliland, lakini mkoa bado una maktaba chache sana za umma na vitabu vingi vya kiada vinachapishwa kwa lugha nyingine ambazo si Kisomali, alisema Khadar Abayare, profesa wa Chuo Kikuu cha Hargeisa.

Hargeisa ina maktaba mbili pekee ambazo zinatumiwa na umma: Maktaba ya Umma ya Gandhi inayoendeshwa kibinafsi na kituo kinachoendeshwa na Mfuko wa Asasi ya Kiingereza kwa ajili ya Elimu ya Afrika, alisema Hodo Sultan Aden, mkuu wa Shirika la Mohamed Mogeh kwa ajili ya Kusoma, Kuandika, Mila na Utamaduni.

"Kusoma ni kipengele muhimu ambacho kinakosekana sasa, na wanafunzi wanazuiliwa katika ufafanuzi wanaopewa na walimu," Aden aliiambia Sabahi. "Hii ni changamoto ambayo inazuia ubora wa ukuaji wa kujifunza wa wanafunzi wa Chuo Kikuu huko Somaliland."

Post a Comment

أحدث أقدم