Rais wa Cyprus, Nicos
Anastasiades, anatarajiwa mjini Brussels kufanya mazungumzo kuhusu hatua
za kuinusuru nchi yake isifilisike.
Bunge liliamua kuweka vikwazo juu ya biashara za fedha na kuanzisha mfuko wa kutafuta michango kusaidia pato la nchi, wakati nchi inajaribu kutimiza shuruti iliyowekewa na Umoja wa Ulaya kabla ya kupata mikopo ya kimataifa.
Kati ya mabadiliko ni kwamba mabenki yatagawiwa pande mbili ili kuwatenga wateja wenye akiba kubwa, ambao waandishi wa habari wanasema, huenda wakapoteza fedha zao nyingi.
Lakini mbunge Prodomos Prodromou wa chama tawala cha Conservative alisistiza kuwa siyo matajiri pekee wataoathirika na mpango huo:
"Matokeo ya hatua hizi yanaonekana mabara-barani.
Mara tu watu wengi wamepoteza kazi zao, na wakati huohuo watu hao watapoteza pesa zao, akiba yao ilioko benki.
Wengine wanaweza hata kupoteza akiba yao ya uzeeni."
إرسال تعليق