Homa ya Kuwa na Makalio Makubwa Inavyowatesa Wanawake


Mwanadada Vanity Wonder ameamua kuandika kitabu kusimulia kwa nini aliamua kutumia kiasi cha dola 15,000 kuchoma sindano za kukuza makalio.

Vanity mwenye miaka 30 mama wa watoto wa wawili wa nchini Marekani kabla alikuwa mwembamba tu hana makalio.

Anasema wanawake wengi hufikia hatua hiyo sio kwa lengo la kuwavutia wanaume bali kutoridhika na anachokiona kila anapojiangalia kwenye kioo.

Vanity anavyoonekana sasa baada ya kukuza hips na makalio.Anasema ameamua kuandika kitabu kuelezea ukweli kwa nini aliamua kufanya hivyo.

Anasema kuwa kwenye process wanawake wengi hupoteza maisha,hupata ulemavu wa kudumu na matatizo mengi tu hutokea.Wanawake wengi kisa kamuona mtu fulani kafanikiwa kukuza makalio hupata tamaa matokeo yake huenda kwa wataalam wa vichochoroni kukwepa gharama.Matokeo ndio huwa vifo na ulemavu

Post a Comment

Previous Post Next Post