Mandela aombewa afya njema

Waumini Afrika kUsini wakimuombea Mandela
Makanisa ya Afrika Kusini yamemuombea rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anatibiwa homa ya mapafu, pneumonia.
Jumamosi msemaji wa rais, Mac Maharaj, alieleza kuwa Bwana Mandela aliweza kuvuta pumzi bila ya shida na amepata nafuu, lakini bado wasi-wasi ungaliko kuhusu kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 94.
Bwana Mandela aliishi mtaa wa Soweto, Johanneburg, kwa miaka mingi.
Mkaazi mmoja wa Soweto, Eddie Vilakazi, aliyemuombea Bwana Mandela katika ibada ya Pasaka Jumapili, anasema anatumai mzee huyo ataishi muda mrefu:
"Mandela ni kiongozi wetu.
Tunamuona kuwa mkombozi wetu.
Ni kila kitu kwetu.
Tunamtakia afya njema haraka.
Mungu amuangalie, ambariki kwa sababu tayari ameshabarikiwa.
Lakini tunamtakia maisha marefu zaidi, awe nasi."

Post a Comment

Previous Post Next Post