Mashabiki wa Al-Ahly wakihamaki baada ya hukumu ya kifo kwa
wenzao kuidhinishwa leo kutokana na vurugu za Uwanja wa Port Said mwaka
jana
MASHABIKI wa klabu ya Al-Ahly ya Cairo,
wamevamia ofisi za Shirikisho la Soka Misri makao makuu na kuzichoma
moto kwa hasira za wenzao kuhukumiwa kifo kutokana na vurugu za mwaka
jana kwenye Uwanja wa Port Said.
Mapema leo, Korti ya Cairo imethibitisha
hukumu ya kifo waliyopewa mashabiki wa soka 21 kutokana na kuhusika na
vurugu hizo, ambazo zilisababisha vifo vya watu 74 na wengine 1,000
kujeruhiwa.
Moto pia ulifika hadi kwenye kituo cha
Polisi jirani, lakini haijajulikana kwa uhakika kama ni mashabiki wa
Al-Ahly waliohusika na tukio hilo.
Ndani ya Cairo, mashabiki wa Al-Ahly wakichoma moto ofisi za shirikisho
Jamaa akilalamikia uamuzi wa korti leo kuhusu tukio la vurguu
kwenye Uwanja wa Port Said mwaka jana. Wengi wa waliohukumiwa kifo ni
mashabiki wa Al Masry
Post a Comment