MAAFISA SITA WA JESHI LA POLISI WASIMAMISHWA KAZI KUTOKAKANA NA SABABU ZA KUPOKEA RUSHWA.

Jeshi la polisi nchini limewasimamisha kazi maafisa wake sita wa jeshi hilo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo za kuwabambikizia wananchi kesi zisizo na dhamana kutokana na rushwa pamoja na kuwa piga.


Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Mambo ya ndani Dk. EMANUEL NCHIMBI, ambapo ambapo amelazimika kutaja baadhi ya Makosa yaliyofanya mpaka kufukuzwa kazi kwa maafisa hao, Ikiwemo sakata la Madawa ya Kulevya liliokuwa limetokea machi Mwaka jana Ambapo madawa ya kulevya yenye Uzito wa kilo 1.9 Yalikamatwa huko Tunduma Mkoani Mbeya na Hatimaye kupelekwa kwa mkemia mkuu na kubainika kuwa Kilichopelekwa kwa mkemia sio madawa bali nichumvi na sukari.


Kutokana na sakata hilo pia Jeshi la Polisi limemueleza Mkuu wake IGP Mwema juu ya kuwasimamisha na hatimaye kuwafungulia mashitaka ya kijeshi wahusika wa sakata hilo.

1.Aliyekuwa mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya - ELIAS MWITA.

2. JACOB KIANGO - Aliyekuwa msaidizi mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mbeya na.

3. CHARLES KINYONGO - Aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya.


WALIOFUKUZWA KAZI POLISI NAKUTAKIWA KUFUNGULIWA MASHTAKA YA KIJESHINI.

1. PETER MATAGI - Aliyekuwa mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kagera., huyu ni kwakosa la kupiga na kuwabambikizia kesi zisizo na dhamana wananchi kutokana na rushwa.

2. PAUL MG"ONG"O - Huyu yeye ni kwakosa la kuingia kwenye hifadhi ya mbuga ya wanyama ya serengeti na kupanga njama ya kuchimba madini aina ya dhahabu ndani ya hifadhi ya serengeti.

Aidha Nchimbi Amemtaja kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Bw RENATUS CHALAMILA aliyekuwa Afisa msimamizi Masuala ya ajira Jeshi la Polisi Amepewa likizo ya mwezi mmoja huku kosa lake kwa Rais likisubiri kuwajibishwa kutokana na cheo chake, Anakabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ili kuwapatia nafasi za ajira wananchi ambao walitaka kujiunga na jeshi la Polisi
waliokuwa wanataka kujiunga na jeshi hilo.

Post a Comment

أحدث أقدم