Maombi Ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare Yapangiwa Jaji

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare akifunguliwa pingu alipofikishwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Picha na Michael Jamson
----
Dar es Salaam. Maombi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare kupinga utaratibu wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kumfutia mashtaka kisha kumkamata na kumfungulia tena mengine, tayari yamepangiwa jaji wa kuyasikiliza.
Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na mmoja wa mawakili wanaomtetea Lwakatare, zinadai maombi hayo yamepangwa kusikilizwa na Jaji Lawrence Kaduri. Hata hivyo, tarehe ya kusikilizwa kwa maombi hayo haijapangwa.

Lwakatare anayekabiliwa na kesi ya ugaidi na mwenzake Ludovick Joseph, kupitia kwa jopo la mawakili wanaomtetea, wiki iliyopita aliwasilisha maombi Mahakama Kuu Dar es Salaam akipinga uamuzi wa DPP kuwafutia mashtaka kisha kuwakamata na kuwafungulia tena mashtaka hayo.

Siku hiyohihyo alipowasilisha maombi hayo, Mahakama Kuu ilitoa hati ya kuita majalada yanayohusiana na kesi yao, ikiiamuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iwasilishe majalada hayo mahakamani hapo.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea.......>>>>

Post a Comment

Previous Post Next Post