
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred
Lwakatare akifunguliwa pingu alipofikishwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Picha na Michael
Jamson
----
Dar es Salaam. Maombi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na
Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare kupinga utaratibu wa Mkurugenzi wa
Mashtaka (DPP) kumfutia mashtaka kisha kumkamata na kumfungulia tena mengine,
tayari yamepangiwa jaji wa kuyasikiliza.
Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na mmoja wa
mawakili wanaomtetea Lwakatare, zinadai maombi hayo yamepangwa kusikilizwa na
Jaji Lawrence Kaduri. Hata hivyo, tarehe ya kusikilizwa kwa maombi hayo
haijapangwa.
Lwakatare anayekabiliwa na kesi ya ugaidi na mwenzake Ludovick Joseph, kupitia kwa jopo la mawakili wanaomtetea, wiki iliyopita aliwasilisha maombi Mahakama Kuu Dar es Salaam akipinga uamuzi wa DPP kuwafutia mashtaka kisha kuwakamata na kuwafungulia tena mashtaka hayo.
Siku hiyohihyo alipowasilisha maombi hayo, Mahakama Kuu ilitoa hati ya kuita majalada yanayohusiana na kesi yao, ikiiamuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iwasilishe majalada hayo mahakamani hapo.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea.......>>>>
إرسال تعليق