
Wolper
Kajala anakabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha haramu kwa kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa kushirikiana na mumewe, Faraji Agustino.
kajala
Kwa
mujibu wa mwigizaji mmoja maarufu wa kiume, tayari ujumbe mfupi wa
maandishi (SMS) na ujumbe kupitia mitandao ya kijamii umeanza kusambazwa
kwa baadhi ya mastaa hao ambao kila mmoja anaonesha kuwa tayari kwa
ishu hiyo ya kumuomba Mungu amsaidie Kajala.
Ray
Mwigizaji huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe,
alidadavua kuwa wanachotafuta kwa sasa ni mahali au nyumba ya ibada kwa
ajili ya kufunga na kumwombea Kajala kuanzia saa 2:00 usiku hadi
asubuhi.
Cathy
“Mwanzoni ilikuwa ni kuhamasishana tu kumkumbuka Kajala katika sala
zetu za kila siku kama ilivyokuwa kwa Lulu (Elizabeth Michael), lakini
sasa tumeona ni vema tukakutana kwa pamoja tumlilie Mungu ili hukumu
yake imuendee vizuri,” alisema mwigizaji huyo na kuongeza:
Lulu
“Yah! Kajala anatia huruma sana ndiyo maana kuna wasanii ambao ni
watu wa karibu yake, wapo tayari kwa ajili ya mkesha wa maombi kama
(Jacqueline) Wolper, Irene Uwoya, Patcho Mwamba, JB (Steven Jacob), Ray
(Vincent Kigosi), Richie (Single Mtambalike), Dude (Kulwa Kikumba) na
wengine wengi.”
Jb
Katika kesi hiyo iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Kajala
amesota Segerea kwa takribani mwaka mmoja ambapo sasa hatma yake
itajulikana tarehe tajwa hapo juu.
Post a Comment