
Mke wa
Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa wakiwasili kwenye hafla ya harambee
ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya
Butiama mkoa wa Mara chini ya Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la
Kiabakari,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini
Dar es Salaam.Kushoto ni Rais wa Bodi ya Mradi huo,Dkt. Patrick Mugoya.

Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akizungumza machache kabla ya kuanza harambee ya kuchangisha fedha za
ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara
chini ya usimamizi wa Padri Wojciech Adam (hayupo pichani) wa
kanisa Katoliki la Kiabakari lililopo wilayani humo,Hafla hii
ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es
Salaam.

Padri
Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari akitoa historia fupi ya
mradi huo toka kuanza kwake mpaka walipofikia wakati wa hafla
ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo
katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara,iliyofanyika mwishoni mwa wiki
kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.ambapo Mgeni Rasmi katika
harambee hiyo,alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.

Mbunge
wa Jimbo la Musoma Vijijini,Mh. Nimrod Mkono akizungumza machache
wakati wa kukabidhi mchango wake na kuahidi kuendelea kuchangia ili
kuhakikisha ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa
wa Mara inafanikiwa huku akisikilizwa kwa makini na Mgeni Rasmi wa
Harambee hiyo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh.
Edward Lowassa pamoja na Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,Mh. Nimrod Mkono akikabidhi mchango wake kwa Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere huku akisaidiwa na Mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.

Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akimkaribisha Brigedia Jenerali,Zoma Kongo kukabidhi mchango wake kwa
Mama Maria Nyerere kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara.

Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Mhariri
Mtendaji wa Kampuni ya Free Media,Ansbert Ngurumo ampa mkono Mama Maria
Nyerere mara baada ya kutoa ahadi yake ya kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara.

Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akimkabidhi picha Boss Mkuu wa Mgahawa wa BreakPoint mara baada ya
kununua kwenye mnada aliouendesha yeye mwenyewe.Katikati ni Mke wa Baba
wa Taifa,Mama Maria Nyerere.

Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,Mh. Nimrod Mkono.

Rais wa Bodi ya Mradi huo,Dkt. Patrick Mugoya akizungumza machache kwenye hafla hiyo.

Meza kuu.

Mke wa
Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere (kushoto) na Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) wakiwa kwenye
hafla ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika
wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya Padri Wojciech Adam (katikati)
wa kanisa Katoliki la Kiabakari,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye
hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.




Wadau Mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo.
Habari na Picha Na:- http://michuzi-matukio.blogspot.com

إرسال تعليق