Rapper
Hamis Mwinjuma aka Mwana FA ambaye March 13 mwaka huu alisherehekea
siku yake ya kuzaliwa, ameiomba serikali kuwafikiria mara mbili mbili
wasanii na kuachia mifumo yote miwili ya digitali na analojia kwakuwa
mfumo wa digitali unawaumiza.
Akiongea na gazeti la Habari Leo, FA amesema kwa sasa wasanii nchini wanaumizwa na mfumo wa digitali kwakuwa wamekuwa wakitumia fedha nyingi katika kutengeneza video, lakini zinaishia kutazamwa na watu wachache tu wenye ving’amuzi.
“Waachie mifumo yote kwani kila mtu atakuwa na uamuzi wa kufanya, kutokana na ubora wa kazi,” alisema Mwana FA.
Alisisitiza kuwa huenda akasubiri hata miezi miwili na zaidi, kama serikali itakubali kuachia mifumo yote miwili wa digitali na analojia, na kama hawatotaka, basi ataachia hivyo hivyo kwa kuwa hawezi kukaa nayo ndani.

إرسال تعليق