Na
Ezekiel Kamwaga, Kwanza Sul, Angola
TIMU
ya Smba inarejea nchini Tanzania kesho usiku ikitokea Angola ambako jana
ilitolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Libolo ya hapa.
Wachezaji
wa Simba leo asubuhi wamefanya mazoezi katika Uwanja wa Libolo uliopo hapa
ambako mechi hiyo ilichezwa na mchana itasafiri kwenda mji mkuu wa Angola,
Luanda, itakapolala kusubiri safari ya kesho.
Hali
katika kambi ya Simba iliyopo katika Hoteli ya Ritz, ilikuwa ya huzuni kutokana
na kipigo hicho kikubwa zaidi cha ugenini ambacho Simba imewahi kukipata katika
kipindi cha miaka minne iliyopita.
Mara
ya mwisho Simba kupata kipigo kikubwa ilikuwa mwaka 2009 ilipofungwa mabao 5-1
na Harass Al Hadoud ya Misri katika michuano kama hii kwenye mechi iliyopigwa
jijini Alexandria, Misri.
Kwa
ujumla, Simba ilicheza vizuri katika mchezo huo isipokuwa katika dakika 10 za
mwisho ambazo iliruhusu mabao matatu kati ya manne iliyofungwa.
Hata
hivyo, matokeo hayo ya 4-0 hayatoi tathmini halisi ya mechi hiyo kwa vile
katika sehemu kubwa ya mchezo huo, Simba na Libolo zilikuwa zimetoshana nguvu.
Libolo
walikuwa na faida ya kuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa mechi za
kimataifa kama vile kiungo Ruben aliyekuwa nyota wa mchezo huo ambaye pamoja na
kufunga bao la tatu, ndiye aliyekuwa akiichezesha timu hiyo.
Ruben
ametoka kuichezea klabu ya Braga ya Ureno iliyokuwa ikishiriki katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya na tofauti za wachezaji kama hao na wale wa Simba ilionekana
katika namna ambavyo wenyeji walitumia nafasi zao.
Saa
moja kabla ya mechi kuanza, mvua kubwa ilinyesha katika mji wa Calulo na
kuathiri hali ya uwanja jambo lililosabisha mpira kuchezwa katika mazingira
magumu.
إرسال تعليق