
Tunapenda kuutaarifu umma ya kuwa kuna genge la watu
wanaotumia jina la mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata katika mtandao wa
kijamii wa Facebook ili kuwarubuni wasichana. Kuna ukurasa ujulikanao kama Flaviana Matata’s hutumika kama moja ya
ukurasa wa Mwanamitindo huyu kitu ambacho si kweli. Watu hawa huwarubuni
wasichana na kuwaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi kwa mgongo wa Mwanamitindo
huyu. Genge hili la uhalifu hudai kuwa
kuna ‘kaka’ yake Flaviana ambaye hukutana na wasichana hawa na baada ya
mazungumzo anawalaghai kwa njia mablimbali. Pia wahusika hawa hutoza kiasi cha
pesa hata kufikia shilingi laki mbili (200,000 )kama tozo kwa huduma hii ya kuwatafutia kazi nje ya
nchi.

Compass Communications kama kampuni inayosimamia shughuli za
Flaviana Matata inatoa tahadhari kwa umma kuwa Flaviana Matata hahusiki kwa
njia yoyote na ukurasa huu au watu hawa.
Pia
tunawatahadharisha wananchi kuwa wawe waangalifu kwani Flaviana Matata hayuko
katika biashara ya kumtafutia mtu yoyote kazi ya Uanamitindo popote pale.
Ukurasa halisi ya Flaviana Matata kwenye mtandaomwa Facebook
ni “Flaviana Lavvy Matata” .
Hivi sasa tunaendelea kushirikiana na vyombo husika kwa
kutoa taarifa kuhusu uhalifu huu na tunaomba ushirikiano wenu pia Wanajamii.
Imetolewa na
Compass Communications
إرسال تعليق