
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkoa
maalum wa vyuo vikuu, kanda ya Dar es salaam, umefanya kikao cha
kujadili mipango na mikakati mbalimbali ya kuimarisha Mkoa huo na Chama
kwa ujumla.
Pamoja na Ajenda hiyo, pia kikao hicho:-
· Kimelaani
vikali matukio ya kuvamiwa, kudhuru mwili na kuuawa kwa baadhi ya
viongozi wa Dini na wanahabari. Mkoa umesikitishwa sana na tukio la
kushambuliwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri Mtendaji
wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda.
· Lakini
pia, kimevitaka vyombo vya Dola kuwakamata, kuwashikilia na
kuwachukulia hatua za kisheria wote waliothibitika kuhusika na matukio
ya namna hiyo bila kuangalia Itikadi za Kivyama, Cheo ama Kundi. Na pia
kuyataka makundi ya kijamii, wanaharakati na wanasiasa kuacha
kuingilia/kuvuruga kwa namna yeyote taratibu za kisheria na kiusalama.
· Pia,
kuwataka wanausalama kumhoji kwa kina Dr Slaa juu ya tuhuma zake dhidi
ya Kurugenzi ya Usalama wa Taifa (TISS) na kumtaka kuthibitisha madai
yake kuwa baadhi ya watendaji wa taasisi hiyo muhimu na nyeti wanaripoti
kwake kinyume cha utaratibu, kanuni na maadili ya taasisi hiyo.
Kwani
tuhuma hizo ambazo Dr Slaa amekuwa akizisema mara kwa mara tangu
kipindi cha Kampeni za Urais Mwaka 2010 zimeanza kuaminika, lakini pia
zimepelekea wananchi sasa kukosa imani na Taasisi hiyo na zaidi kupoteza
imani juu ya uwezo wa serikali kuwalinda na kuwahakikishia Usalama wa
maisha yao, ambapo ni jukumu la kikatiba la serikali.
إرسال تعليق