TAMKO LA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi:'KUHUSU GOROFA PACHA KARIBU NA LILILOANGUKA

 ''Watu waliyoko karibu na jengo jingine la ghorofa 15 lililojengwa na mkandarasi wa kwanza aliyejenga jengo la ghorofa 16 na Kuporomoka Nakusababisha vifo vya Watu 22 ,kuhama mara moja na ubomoaji ufanyike bila kuleta madhara.'
 
Picha Juu ni jengo jingine la ghorofa 15 lililojengwa na mkandarasi aliyesababisha jengo la ghorofa 16 kuanguka na kusababisha vifo vya watu 22 hadi sasa ambalo waziri lukuvi ametoa maelekezo kubomolewa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi
---
Dar es Salaam. Idadi ya watu waliokufa kutokana na kufukiwa na kifusi cha jengo la ghorofa 16 lililoporomoka juzi asubuhi jijini Dar es Salaam, imefikia 22.
Habari zilizopatikana kutoka eneo la uokoaji na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova zinaeleza kuwa miili iliyopatikana imepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Post a Comment

Previous Post Next Post