AZAM WAENDELEA NA MAZOEZI

Mabingwa wa mapinduzi cup azam fc leo asubuhi wameendelea na mazoezi baada ya kuwapa mapumziko ya siku mbili wacgezaji wa timu hiyo mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam jumamosi ya machi 30 wakitokea Kibaha kuwakabili ruvu shooting katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom.
Azam wanajianda na mchezo wa kombe la shirikisho utakaocheza katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam siku ya jumamosi saa kumi na nusu dhidi ya Barack YC II ya Liberia.
Barack YC wamewasili jijini Dar es salaam leo asubuhi teyari kwa mchezo huo wa marejeano, baada ya ule wa awali uliochezwa Monrivo Liberia na kumalizika kwa azam kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Mwamuzi wa kati katika mchezo huo ni Adelaide Ali, akisaidiwa na Amaldine Soulaimane na Ibrahim Mohame. Wakati Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ansudane Soulaimane.
Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni atakuwa Abdelhamid Radwan kutoka Misri. Maofisa hao wa mechi hiyo watafikia kwenye hoteli ya Holiday Inn.

Post a Comment

Previous Post Next Post