
Mabingwa
wa mapinduzi cup azam fc leo asubuhi wameendelea na mazoezi baada ya
kuwapa mapumziko ya siku mbili wacgezaji wa timu hiyo mara baada ya
kuwasili jijini Dar es salaam jumamosi ya machi 30 wakitokea Kibaha
kuwakabili ruvu shooting katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom.
Azam
wanajianda na mchezo wa kombe la shirikisho utakaocheza katika uwanja wa
taifa jijini Dar es salaam siku ya jumamosi saa kumi na nusu dhidi ya
Barack YC II ya Liberia.
Barack YC wamewasili jijini Dar es salaam
leo asubuhi teyari kwa mchezo huo wa marejeano, baada ya ule wa awali
uliochezwa Monrivo Liberia na kumalizika kwa azam kuibuka na ushindi wa
goli 2-1.
Mwamuzi wa kati katika mchezo huo ni Adelaide Ali,
akisaidiwa na Amaldine Soulaimane na Ibrahim Mohame. Wakati Mwamuzi wa
mezani (fourth official) ni Ansudane Soulaimane.
Kamishna wa mechi
hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni atakuwa Abdelhamid Radwan kutoka
Misri. Maofisa hao wa mechi hiyo watafikia kwenye hoteli ya Holiday Inn.
إرسال تعليق