Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana jioni hii ni haya yafuatayo baada ya kuongea na Mwanasheria wa Lema wakili Humphrey Mtui

i)Kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting for)

ii)Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’Kwa hiyo huo ni uchochezi

iii)Kosa la Tatu ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’Huu nao umeitwa kwamba ni uchochezi.

Sasa haya maneno hapo juu ndiyo yaliyosababisha jeshi la polisi kuvamia nyumbani kwake usiku wa manane na kuzua taharuki maeneo hayo na ndani ya nyumba yenye ndugu jamaa na hata mtoto mwenye miezi mitano huku polisi wakitumia nguvu na kukiuka sheria

Huo umeitwa uchochezi baada ya mkuu wa mkoa kumtumia ujumbe wa mkononi kupitia simu yake kupitia namba 0752960276 aliyotishia kumbambikizia kesi anayoitaka yeye.

Sasa hayo waliyoita makosa ya uchochezi ndiyo yaliyomnyima haki ya dhamana leo.tutafakari kama Arusha itatawalika kwa hali hii.

Hebu tupime makosa hayo matatu kama yanaweza ku-justfy mambo yote yaliyotokea.