Facebook imekuwa kama Google ya mitandao ya
kijamii. kama sasa hivi hauposti status yako basi unapandisha picha au
unajibu quiz ya facebook games. Tunaandika vitu vya ndani kabisa vya
maisha yetu ambavyo katika maisha halisi hatuwezi kumwambia yoyote.
Tunadhani kwamba ili mradi tumeweka privacy settings zetu sawa sawa
basi tupo salama.
tatizo ni kwamba hatujui nani
hasa anatuchunguza habari zetu. Akaunti ya rafiki zatu inaweza ikawa
hacked baada ya kuweka program ya ajabu ajabu kwenye simu au computer,
au labda mjomba wake ndio anatumia account kwa sababu amesahau ku-log
out. lakini vile vile ni internet cafe ambapo wabongo wengi
tunapapendaKwa usalama wako na wa familia yako, kuna vitu haupaswi
kuviandika Facebook. Kamwe. Hivi hapa ni vitu vitano ambavyo inabidi
uvitoe au siviandike kwenye Facebook.
1. Tarehe yako ya kuzaliwa yote kamili.
Sote
tunapenda kupata Happy birthday notifications kwenye walls zetu.
Inatufanya ndani ya moyo tujisikie raha fulani kwamba kuna mtu
amekumbuka birthday yako na amekutumia wishes. Tatizo ni kwamba
unapoweka mwaka wako wa kuzaliwa wote, unawapa wezi nafasi ya kupata
moja ya taarifa za muhimu zinazohitajika ili kukuibia. Ni muhimu
usiweke na kama ukiamua kuweka basi usiandike mwaka wenyewe. Kwanza
marafiki zako halisi wanajua tayari.
2. Hali yako ya mahusiano
Uko
kwenye mahusiano au la, ni vyema usiutangazie umma. Stalkers
watafurahia kujua kwamba kuna single mpya mtaani.Ukibadilisha status
yako kuwa single ndio umewawashia taa ya kijani kwamba umerudi sokoni.
Kama ulikuwa umeoa ndio utafanya wajue kuwa upo nyumbani peke yako. Cha
busara kufanya ni kutokuandika kabisa.
3. Mahali ulipo
Kuna
watu wengi wanapenda ile feature ya facebook ya location tagging
ambapo unaweza kum-tag mtu/watu kwamba uko wapi. Tatizo ni kwamba
umeshawaambia watu kwamba upo likizo mkoa na sio nyumbani kwako. Tena
ukiongeza utakaa muda gani basi wezi/majambazi ndio watajua kabisa ni
mmuda gani wakavamie kwako. Ushauri wangu ni kwamba usiandike kabisa.
Unaweza kuweka picha zako za safari ukisharudi nyumbani.
4. Kwamba upo nyumbani peke yako
Wasichana
wengi wa kibongo ndio wanapenda hii. "Nipo nyumbani peke yangu
nimeboreka kweli!" "Nipo lonely nyumbani, nipeni ushauri fans wangu" na
vitu kama hivyo ndio utavikuta kwa waTZ wa facebook wengi.
Tunaweza
tukadhani ni marafiki wetu tu ndio wanaona post zetu, lakini ukweli ni
kwamba hatuwezi kujua nani anasoma tarifa zetu. Mtu anaweza kuiba
akaunti ya rafiki yako mradi apate mwanya wa taarifa zako! Unaweza
ukaweka privacy settings lakini kama account ya rafiki yako
ikichezewa, kila kitu kipo wazi.
5.Picha za wanao na tags za majina yao
Wenye
watoto mnapenda watoto wenu.Mtafanya chochote kuwalinda na kuwaweka
salama. lakini wengi huweka picha za wanao ndani ya facebook na wengine
huenda mbali mpaka kuweka picha za wanao kama profile picha!
Wazazi
9 kati ya 10 wameshawahi kuweka picha za wanao na majina yao na
wengine kuwa-tag na ndugu, marafiki, na jamaa zao. Taarifa kama hizi
zinaweza kutumiwa na wahuni kukuumiza wewe. Wanaweza kutumia jina la
mwanao na la ndugu kujenga uaminifu na kumshawishi mwanao kuamini
kwamba wao sio watu wabaya au wageni kwenye maisha yake kwa sababu "ona
mpaka najua ndugu zako wote na marafiki zako mpaka mama yako na baba
yako nawajua!"
Kama kuna haja ya kuweka picha zao
basi usiandike majina yao kamili na tarehe zao za kuzaliwa. marafiki
zako wa kweli hata hivyo si wanamjua mwanao tayari?
Najua
wazazi wengi wanajivunia watoto wao na wanatamani dunia nzima wajue
kuwa wanawapenda wanao. Lakini "Kama kweli unampenda, utamlinda".
Chanzo:tanganyikanblog
إرسال تعليق