
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema na Mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mnyika
---
Wakati Bunge la 11 la Bajeti kwa mwaka huu likianza kesho,
Kamati Kuu ya Chadema imesema itatumia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
kulibana Bunge kuhusu utendaji usiofuata Kanuni za Bunge unaofanywa na
Spika na wasaidizi wake.
Pia wabunge hao wameitaka Serikali kuweka wazi
mikataba iliyoingia hivi karibuni na Serikali ya China ili wananchi
waweze kufahamu kilichomo vinginevyo watatumia kambi hiyo kuwabana
wahusika.
Katika kikao cha 10 kilichomalizika Februari 8,
mwaka huu mjini Dodoma, Mnadhimu wa kambi hiyo, Tundu Lissu alisema kuwa
wanaandaa hoja za kumng’oa Spika na Naibu wake, Job Ndugai kwa kile
walichodai kukiuka kanuni mbalimbali za Bunge.
Kambi ya upinzani ilikuwa ikilalamika kuondolewa
kwa hoja binafsi za baadhi ya wabunge wao ikiwemo ya Mbunge wa Ubungo,
John Mnyika (Maji), James Mbatia (Mitalaa ya Elimu) na Joshua Nassari,
ambaye hoja yake ilihusu utendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa
(NECTA).Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea.......>>>
إرسال تعليق