Ezekiel Maige : Kwa nini nimekataa bajeti ya Kilimo

Wapendwa marafiki, yawezekana wenginenhamjafuatilia mjadala Bungeni leo na hivyo mnaweza kusikia kupitia vyombo vya habari na hivyo kupata edited version of my comments. Nawafahamisha kuwa nimekataa bajeti kwa kuwa Bajeti haijatatua wala kuonyesha mwelekeo wa kutatua matatizo ya wananchi wangu ambayo ni NJAA ENDELEVU kutokana na ukame wa mara kwa mara na UMASKINI unaozidi kuongezeka kutokana na BEI DUNI YA MAZAO YA KILIMO NA MIFUGO NA TIJA NDOGO KATIKA KILIMO. Nilitegemea Bajeti iwe na Skimu zaUMWAGILIAJI kama jibu la mvua haba na pia PRICE STABILIZATION FUND kwa bei ya Pamba. Aidha nilitegemea kungekuwa na mkakati wa kuanzisha viwanda vya nguo ili kuwa na soko la ndani kwa pamba yetu! Sjinyanga, ambayo kila siku kuna njaa hakuna skimu ya umwagiliaji na maeneo yenye mvua kama Kigoma, Rukwa, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya nk yenye mvua ndiyo yamewekewa skimu za umwafiliaji. Hili haliwezekani. NIMEKATAA.

Post a Comment

أحدث أقدم